Na Mwandishi Wetu
Leo, Novemba 20, 2024, Chama cha National League for Democracy (NLD) kitazindua rasmi kampeni zake za uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji, na vitongoji.
Uzinduzi huo utafanyika katika Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, ambapo viongozi mbalimbali wa chama hicho watashiriki. Kampeni zitazinduliwa Kwedkwazu Mashariki, zitaendelea kuhamasisha wanachama na wananchi katika maeneo mengine ya Tanga na nchini kwa ujumla.
"Baada ya November 20, Kampeni za Chama cha NLD zitafanyika nchi nzima hususani mahala ambapo Chama cha NLD, kimesimamisha Wagombea." Alisisitiza Doyo Hassan Doyo Katibu Mkuu wa Chama cha NLD.
Comments