CHAKOR,muigizaji wa tamthilia ya UDAAN sapnon Ki anayopendwa nchini Tanzania
UDAAN sapnon ki ya CHAKOR ILIVYOTIKISA SOKO LA FILAMU NA TAMTHILIA BONGO CHINI YA #DJMURPHY
Jina la binti mdogo muigizaji Spandan Chaturvedi maarufu kama CHAKORII huku wengine wakimuita Chokha bhai siyo ngeni katika masikio na macho ya watanzania wanaopenda kutazama filamu na tamthilia zilizotafsiriwa kwa maneno ya kiswahili hapa bongo binti huyu aliyezaliwa tarehe 25 mwezi agost mwaka 2007 huko Mumbai nchini India mpaka sasa ana miaka Tisa tu lakini tayari ana umaarufu mkubwa .
Sapnon ki UDAAN ambayo ilianza kuonyeshwa na kituo maarufu cha televisheni duniani kinachoonyesha muvi na tamthilia za kihindi COLORS TV mwaka 2014 ambayo inakadiriwa kuwa itamalizika baada ya miaka kumi yaan mpaka 2022 tangu ilipoanza kuonyeshwa katika kituo hicho cha COLORS TV ambapo binti Hugo amecheza katika vipande vya kuanzia mwaka 2014-2016 alipomuachia Chakor Mkubwa imekuwa ni tamthilia pekee ya nje kutikisa Tanzania ambayo imependwa na watazamaji wa rika zote tangu ilipoanza kutafsiriwa na muingiza maneno ya kiswahili aliyejipatia umaarufu siku za hivi karibuni katika mikoa mbali mbali ikiwemo Dar es salaam na Pwani mkali kutoka arusha #DJMURPHY.
Tamthilia hiyo inayozungumzia maisha ya kijiji cha Azadganj, uttar pardesh chini ya mbunge Kamal Nayaran "BHAIYA G" ambaye amewageuza wakazi wa kijiji hicho kama watumwa kwa kuwanunua na kuwaweka alama maalum (mihuri)katika mikono yao
Tamthilia hyo inaaza Mara ambapo tunamuona baba yake Chakor bwana Bhuvan akiwa amekosa fedha kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya baba yake mzazi (babu yake Chakor)aliyefariki kwa ajali ya kuanguka hivyo ikamlazimu Bhuvan na mkewe Kasturi ambaye alikuwa mjamzito wakati huo kwenda kuomba msaada kwa bosi wao Kamal nayaran ambaye wamekuwa wakimtumikia kama watumwa kwa kipindi chote cha maisha yao.
Baba chakor (bhuvan)na mama chakorchakor (kasturi) |
Tajiri kamal narayan a.k.a BHAI G |
Picha linakuwa tamu pale ambapo Mke wa Kamal nayaran,mwanamama Tajaswini anapotoa sharti kuwa kama wanataka msaada wamuuze kwanza kichanga kilicho tumboni "Chakor" ili wapewe fedha ambapo baada ya Mtoto Huyo kuzaliwa angekuwa mtumwa wao na kwa kuwa walikuwa na shida baba na mama yake na Chakor wakatia saini karatasi kuuza kichanga chao kuja kuwa mfanyakazi katika nyumba ya kamal narayan BHAIYA G pindi tu katapozaliwa na kufikisha miaka mitano.
Katika usiku wa mwezi mng'aavu Kasturi akafanikiwa kujifungua Mtoto wa kike na kumpa jina CHAKOR ambaye alipendwa na kijiji kizima kutokana na ucheshi wake na jinsi alivyokuwa akiwakarimu watu katika kijiji kile kila mtu alimpenda sana Chakor wakiwemo watoto wenzake na watu wazima miongoni mwao akiwemo mdogo wake wa kike aitwaye IMLU pamoja na marafiki wengine akiwemo BILU na TILU wakaishi naye kwa muda na hatimaye baada ya miaka saba kupita tajiri na mbunge Kamal narayan Bhaiya G Neill alipomtaka Mtoto huyo ili awe mtumwa nyumbani kwake hapo ndipo story tamu na vituko vya Chakor Mtoto mwenye vituko na akili nyingi inapoanza kunoga "TAFUTA COPY YAKYAKO
Mdogo wake Chakor IMLU |
Hapo ndipo tamthilia hiyo ilipoteka hisia za watu wengi duniani na hata Tanzania na kuzifanya tamthilia nyingine hasa za kikorea na kichina kukosa soko kubwa hapa nchini kwa kipindi ilichokuwa inatoka UDAAN lakini ilikuja kukosa nguvu kubwa Mara baada ya ma DJ wengine kuirukia na kuanza kuitafsiri bila mpangilio kama alivyokuwa anaitafsiri DJ MURPHY lakini mpaka Leo ni tamthilia pekee ambayo umevutia hisia za watanzania walio wengi hasa katika uigizaji wa Mtoto Chakor na imepatua umaarufu mkubwa nchini ukiachana na tamthilia nyinginezo za kihindi zikiwemo Naagin,meri ashq,bandini na nyinginezo zikiwemo za kitanzania.
Ambapo mpaka sasa malkia wa tamthilia hyo binti CHAKOR ameshanyakua tuzo nyingi nchini India na kuwa mwigizaji wa kike aliye chini ya umri wa miaka 18 aliyewavutia zaidi watazamaji wengi wa filamu duniani ikiwemo Tanzania.
Comments