KHEA YAFIKIA WAWEZESHAJI 360, WAKULIMA 1500+ KILIMO IKOLOJIA HAI
KHEA YAFIKIA WAWEZESHAJI 360, WAKULIMA 1500+ KILIMO IKOLOJIA HAI Mradi wa kilimo ikolojia hai unaotambuliwa kwa jina la Kitovu cha maarifa cha Afrika Mashariki umefikia tamati Septemba 30 2026 kwa kuwawezesha wakulima viongozi 360 waliowafikia wakulima zaidi ya 1500 na kuwapa elimu na mbinu za kilimo hai. Wakulima hao viongozi kutoka Tanzania bara mkoa wa Njombe, Kilimanjaro, Songwe, Mtwara na Tanzania bara Unguja na Pemba wamefikiwa na mradi huo na kuwawezesha wakulima wa kilimo ikolojia hai katika maeneo yao kujua mbinu za kilimo hai kwa faida. Akizungumza wakati wa kufunga mradi huo Brigita Didas ambaye ni msimamizi wa miradi Taasisi ya Kilimo hai Tanzania (TOAM) amesema kuwa kumalizika kwa mradi huo kunatoa fursa kwa wanufaika kuendelea kuitumia elimu na mbinu za Kilimo ikolojia hai zilizofundishwa wakati wote wa mradi. Ameongeza kuwa lengo kuu la mradi huo ni kukusanya na kusambaza maarifa ya kilimo hai ngazi ya Afrika maarifa yanayotumika na nchi za ukanda huo, kuyaweka kwen...







