AFARIKI NJE YA BENKI BAADA YA KUAMBIWA MALIPO YAKE HAKUNA.


AFARIKI NJE YA BENKI BAADA YA KUAMBIWA MALIPO YAKE HAKUNA.







Kenya.

Mwanamume mmoja alifariki nje ya benki  moja katika kaunti ya Garissa wakati akingojea pesa za malipo ya wazee, masikini na walemavu

-Familia ya Hassan Haji Keinan 70  ilisema marehemu alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Mataarba kilichoko Hulugho ili kupokea malipo yake kutoka kwa benki -Mzee  huyo anasemekana alipatwa na mshituko baada ya kuambiwa kuwa hakuwa katika orodha ya waliostahili kupokea fedha hizo ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali ya Kenya.

Aidha, mzee huyo alikuwa akitarajia kupokea KSh 8,000 ambazo zilikuwa zimejilimbikiza kwa muda wa miezi minne.

 “ Wakati wake wa kuhudumiwa ulipofika, keshia alimwambia kuwa jina lake halikuwa katika orodha ya waliostahili kupokea fedha hizo. Mzee huyo alianza kutokwa na jasho, akazirai na kuaga dunia alipokuwa akipelekwa hospitali kuu ya Garissa,” alisema mwanawe, Gurshed Hassan

Comments