Uvuvi haramu sasa kudhibitiwa ipasavyo Tanzania

Mwarobaini wa uvuvi haramu sasa kupatikana 

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri Mpina wakati akifungua kongamano la siku nne kwa niaba Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan linalokutanisha Wanasayansi wa Bahari kutoka Ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi (WIOMSA) linalojadili masuala mbali mbali yanayohusu shughuli za Baharini.

Ameeleza kuwa baadhi ya viumbe vya baharini vimekuwa vikitoweka kutokana na shughuli za binadamu kama za uvuvi haramu pamoja na utililishaji wa maji ya sumu baharini.

“Uvuvi haramu, utililishaji wa maji ya sumu kutoka viwandani haya yanachangia kupotea kwa viumbe baharini, ndio maana tumekutana kwenye mkutano huu kujadili ili tuweze kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili,” amesema Mpina.

Amesema katika mkutano huo wadau watajadili mikakati ya namna ya kusaidia kuondokana na changamoto za uvui haramu pamoja utumiaji wa utilishaji wa kemikali hizo akitolea mfano kemikali hatari ya  Zebaki.

“Serikali tutachukua haya mapendezeko yote yatakayotolewa na wadau hawa ili ziweze kuchukuliwa kuondokana na hizi changamoto”amesema Mpina.

Kwa wake Mkurugenzi wa wa Taasisi ya Utafiti wa Madawa ya Binadamu nchini,Profesa Yunus Mgaya ameishauri serikali kusimamia sheria zake ili kuweza kudhibiti vitendo haramu vya uvuvi.

Mkurugenzi wa wa Taasisi ya Utafiti wa Madawa ya Binadamu nchini,Profesa Yunus Mgaya.

“Sheria zipo naishauri serikali itilie mkazo wa nguvu kwenye sheria za uvuvi haramu ambapo itachangia kupunguza vitendo hivi”ameishauri Profesa Mgaya.

Mkutano huo wa siku nne umeanza leo  Oktoba 30,2017. Utamalizika Novemba 4, 2017,umekutanisha wadau mbali mbali kutoka nchi tofauti .

Comments