ATHARI NA FAIDA ZA MATUMIZI YA INTERNET KWA WATOTO

 



Na PrayGod Thadei,Dar es salaam.


Matumizi ya internet kwa watoto yamekuwa yakiongezeka kadiri teknolojia inavyoendelea kukua hata hivyo,Internet imebadilisha jinsi tunavyoshirikiana, kupata habari, na kujifunza, lakini pia ina athari zinazoweza kuathiri watoto kwa njia mbalimbali. Hapa chini nitaelezea makala kuhusu matumizi ya internet kwa watoto na athari zake:


Pande zote za sarafu: Matumizi ya internet kwa watoto yana faida na changamoto zake. Wakati internet inatoa fursa nyingi za kujifunza na mawasiliano, pia kuna hatari za kijamii, kiakili, na kimwili ambazo wazazi na walezi wanapaswa kuzingatia.



Hata hivyo kwa mujibu wa Waziri wa maendeleo ya jamii,jinsia,wanawake na makundi maalum,Dkt Dorothy Gwajima amesema matumizi ya mitandao kwa Watoto hapa nchini yamekuwa na faida na hasara zake kwani huwakutanisha watoto na watu wanaowajua na  wasiowajua ambao wakati mwingine wanaweza kuwa na nia ovu kwao ikiwemo kuwadhuru kiakili,kimwili na kifikra kutokana na watoto kuwa rahisi kurubuniwa kupitia mitandao hiyo.

Aidha Dkt Gwajima anaendelea kwamba faida za kutumia mtandao wa internet kwa ulimwengu wa Sasa ni dhahiri kwamba zipo nyingi lakini zimekuwa pia na madhara makubwa kwa Watoto hivyo jamii inapaswa kuelimishwa juu ya matumizi ya internet kwa Watoto wao huku vyombo vya Habari vikitumika vyema katika kutoka elimu kwa wazazi na walezi kufuatilia mienendo ya watoto wao katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Dkt Gwajima anaendelea kwamba kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2022 watoto Kati ya miaka 12 hadi 17 hapa nchini asilimia 67 wanaitumia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook,TikTok na Instagram, Whatsapp na Telegram ambalo utafiti huo ulionyesha asilimia 4 ya watoto hao walifanyiwa ukatili wa aina mbalimbali ikiwemo kuwasiliana na wahalifu bila wao kujua na kushawishiwa/kulazimishwa kutumia picha za utupu kupitia mitandao.

Waziri Dkt Gwajima pia aliongeza kuwa licha ya mitandao hiyo kuwa na faida lukuki kwa Watoto lakini athari zake pia zimekuwa kubwa kwao kwa kuwapelekea baadhi yao kuanza kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi (ngono) katika umri mdogo Pamoja na kupata athari za kisaikolojia kutokana na mwingiliano wa tamaduni mbalimbali katika mitandao hiyo ambayo watoto wamekuwa wakiiga na kupelekea mmonyoko wa maadili.

Hata hivyo zipo faida za matumizi ya internet kwa watoto endapo watasimamiwa vyema na wazazi au walezi wao Kama vile:
Fursa za kujifunza: Internet inatoa mtandao mkubwa wa rasilimali za elimu ambazo zinaweza kusaidia watoto kuboresha ufahamu wao juu ya mada mbalimbali. Wanaweza kupata maktaba za kielektroniki, vitabu vya elektroniki, na vyanzo vingine vya elimu ambavyo vinaweza kuwawezesha kujifunza masomo mbalimbali.

Kupitia Mawasiliano na utandawazi: Watoto wanaweza kushirikiana na wenzao kutoka sehemu mbalimbali za dunia kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya kijamii. Hii inawasaidia kujenga ujuzi wa kijamii na kukuza uelewa wa tamaduni na mitazamo tofauti endapo tu wataitumia vyema mitandao hiyo.


Hata hivyo kwa mzazi ambaye mtoto wake anatumia mitandao ya kijamii anapaswa kufahamu kuwa Kuna Changamoto na athari za matumizi ya internet kwao kwani kupitia mitandao hiyo pia Kuna Maudhui haramu na hatari kwa Watoto wanaweza kuathirika kisaikolojia,kunyanyaswa kingono,kurubuniwa

Comments