MFUMO WA KUWATAMBUA MADEREVA BODABODA NA BAJAJI KINONDONI WAIVA,KATIBU WAO ASEMA UTAPUNGUZA UHALIFU.
MFUMO WA KUWATAMBUA MADEREVA BODABODA NA BAJAJI KINONDONI WAIVA,KATIBU WAO ASEMA UTAPUNGUZA UHALIFU.
Katibu wa Chama Cha madereva bodaboda na bajaji Wilaya ya Kinondoni Paulo Merlis Zimani akizungumza na waandishi wa Habari. |
Na Mwandishi wetu
Katibu wa Chama Cha madereva wa bodaboda na bajaji Wilaya ya Kinondoni Paulo Merlis Zimani amesema wameweka mikakati Mbalimbali ikiwemo kuja na mfumo mpya wa utambuzi wa madereva na vituo vyao,kote Wilayani humo.Katibu huyo aliyasema hayo kando ya Mkutano uliowakutanisha madereva wa bodaboda na bajaji uliokuwa na lengo la kuangalia changamoto zao na kuanza kwa Mchakato wa urasimishaji wa vituo ndani ya Wilaya ya Kinondoni.
Zimani alisema kuwa vituo vyote vya Wilaya hiyo vitarasimishwa na kuwekewa mabango maalum ambayo pia yatakuwa na idadi ya madereva wanaopatikana kwenye kituo husika pamoja na picha zao.
"tumeitwa hapa kwa ajili ya urasimishaji wa Vituo na Mkurugenzi ameshatuelekeza Kuwa Kila kituo tujue tuna madereva wangapi,na maafisa usafirishaji wangapi na Kila kituo ni lazima tukiwekee bango ambalo litawaonyesha madereva wote wa kituo hicho na hakutakuwa na dereva mwingine yoyote ambaye hana usajili wa eneo lile kuingia kwenye kituo,kwa nini tunafanya hivi ni kwa sababu ya kuondoa malalamiko mengi ya madereva juu ya viongozi wa vituo kuchukua hela za madereva ili kuwapachika vituoni hivyo kama kutakuwa na dereva ambaye anataka kuingia kituoni inatakiwa wote wajue na kama Kuna ada anatoa iwafaidishe madereva wote wa kituo"alisema
Kuhusu uwepo wa malalamiko ya kuwepo kwa baaadhi ya watu wasio waaminifu 'Vishandu' ambao wamekuwa wakitumia boda boda Kufanyika uhalifu kwa kuibia watu barabarani ikiwemo kupora simu na mikoba,Bw Zimani alisema uhalifu huo haufanywi na madereva bodaboda na bajaji na unafanywa na watu wengine wahalifu.
"nikwambie ndugu Mwandishi,watu wengi wanaofanya uhalifu yaani Vishandu siyo madereva wa bodaboda Wala bajaji bali ni watu ambao wako Mtaani wanamjua Kabisa Fulani ana bodaboda wanaenda kuomba Kuwa Kuna mahali wanaenda na huchukua bodaboda hizo na kwenda kufanya uhalifu bila mwenye bodaboda/bajaji kujua Kuwa bodaboda yake imeenda kufanyiwa uhalifu na umakini wa tasnia yetu hakuna dereva anaweza kwenda kufanya uhalifu na tayari bodaboda imeshakuwa ni ajira rasmi ambayo vijana wengi wamejiajiri ambayo inafanya familia na ndugu zake waishi"alisema
Alisema ili kuukabili uwepo wa Vishandu wamekuja na Mikakati Mbalimbali ikiwemo mavazi maalum ya madereva hao ambayo yatakuwa na namba zao za utambuzi kwa kuwaingiza kwenye mfumo maalum (kanzidata) ya kuwatambua na tayari wameanza kushirikiana na jeshi la polisi ili kukomesha tabia hiyo huku akiwataka ambao wanaofanya uhalifu kwa kutumia bodaboda waache mara moja kwani hawatokuwa salama kwa kufanya uhalifu Kinondoni.
Kuhusu uwepo wa mikopo ya vyombo vya moto ikiwemo bodaboda na bajaji Zimani alisema kuwa tayari wameshatoa zaidi ya bodaboda miambili na bajaji kwa vijana kwa kukopeshwa na moja ya Benki hapa nchini ambapo kijana anaweza kutoa Shilingi Laki moja na nusu kama kianzio na kisha kukopeshwa bodaboda ambayo atafanya marejesho ya Shilingi elfu nane Kila siku kwa muda wa mwaka mmoja huku akiwataka vijana wanaohitaji mikopo hiyo kufika kwenye Ofisi za Chama Cha madereva wa bodaboda na bajaji Wilaya ya Kinondoni zilizopo katika soko la Bwawani,Mwananyamala kwa Maelezo zaidi.
Comments