Skip to main content

ELIZABETH MICHAEL "LULU" ATANGAZWA BALOZI WA KAMPUNI YA LUMINA SKIN

 

ELIZABETH MICHAEL "LULU" ATANGAZWA BALOZI WA KAMPUNI YA LUMINA SKIN



NA MWANDISHI WETU

MUIGIZAJI maarufu Elizabeth Michael  "Lulu" ametangazwa kuwa balozi wa Kampuni ya Lumina Skini inayojihusisha na uuzaji wa bidhaa zangozi.

Akizungumza wakati wa utambulisho huo jana jijini Dar es Salaam Meneja Masoko wa kampuni hiyo Osmunda Ndimbo amesema wamechagua kufanya kazi na Lulu kwasababu ni msanii anayependa urembo.

“Tumemchagua Elizabeth Michael kwa sababu ni mpenzi wa urembo na anajali ngozi yake. Bidhaa hizi tumezitengeneza kwa malighafi kutoka maeneo mbalimbali, ingawa bidhaa imetengenezwa China,”. Alisema.

Kwa upande wake, Lulu amesema amekubali kushirikiana na Lumina baada ya kuona ni kampuni yenye mwelekeo mzuri katika tasnia ya urembo.

“Tulianza mazungumzo miezi sita iliyopita. Nilifanya majaribio ya bidhaa kwa mwezi mmoja na niliporidhika, nikaona ni salama na bora kwa wateja,

“Hii ni kampuni ya kwanza kushirikiana nami kwenye eneo la vipodozi. Nilihakikisha wamejisajili kwa sababu afya ya mteja ni kipaumbele,” amesema.

Aliongeza kuwa jina Lumina limetokana na neno la Kilatini lenye maana ya light au mwangaza, kwa lengo la kumpa mwanamke kujiamini bila kubadili asili yake.

“Bidhaa hizi hazichubui wala kuleta mabadiliko yoyote kwenye mwili, na zimetengenezwa kwa viwango vinavyotumika kwenye mataifa makubwa,” alifafanua Lulu.

Comments