Skip to main content

AAFP KUJENGA BWAWA LA MAMBA IKULU LA KUADHIBIA MAFISADI,WAKISHIKA DOLA

 

AAFP KUJENGA BWAWA LA MAMBA IKULU LA KUADHIBIA MAFISADI,WAKISHIKA DOLA





NA MWANDISHI WETU

CHAMA cha Alliance for African Farmers Party (AAFP) kimesema endapo kitapata ridhaa ya kuongoza nchi, kitajenga bwawa maalum lenye Mamba kwa ajili ya kutoa adhabu kali ya kuwatumbukiza ndani ya bwawa hilo mafisadi.

Hayao yamebainishwa leo Septemba 17, 2025 na mgombea Urais wa Chama hicho, Kunje Ngombale-Mwiru, akizungumza na wananachi katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam.

Mwiru amesema hatua hiyo ni ya ishara katika kupambana na rushwa, akisisitiza kuwa adhabu kali kwa watuhumiwa wa ufisadi ni jambo linalowezekana ikiwa kutakuwa na dhamira ya kweli ya kisiasa.

"Haiwezekani mtu kala hela za umma, anatembea na kitambi chake mtaani tunamwangalia tu huku hospitali watu wanakufa kwa kukosa dawa, hiyo sio kwa Serikali yangu.

"Pale Ikulu nitachimba bwawa la mamba na wale mafisadi wote watadumbukizwa, huko kuliwa hadi kuisha na nguo zake mtazikuta zimewekwa hapo kama ushahidi wa hilo kujua kuna mtu alidumbukizwa humo.

"Pia, hiki kirungu changu nilichoshika mkononi kitatumika kuwapiga kabla hawajaingia ndani ya bwawa hilo na kama nina ziara nje ya nchi siku hiyo nitaiahirisha hadi nihakikishe nimemshughulikia fisadi huyo," amesema mgombea huyo.

Comments