Skip to main content

KAMPUNI YA GULF JOBS HUNTS TANZANIA YATANGAZA NEEMA ZA AJIRA FALME ZA KIARABU KWA WATANZANIA ,YAFUNGUA OFISI DAR

 

KAMPUNI YA GULF JOBS HUNTS TANZANIA YATANGAZA NEEMA ZA AJIRA FALME ZA KIARABU KWA WATANZANIA ,YAFUNGUA OFISI DAR




NA MWANDISHI WETU

ILI Kutatua changamoto za ajira nchini,Kampuni ya Gulf Jobs Hunts Tanzania imezinduliwa rasmi nchini ili kutoa fursa za ajira kwa vijana wa Kitanzania kwenda kufanya kazi katika nchi mbalimbali za Umoja wa Falme za Kiarabu zenye Dubai, Abudhabi, Alain, Ras Alkhima, Sharjah, Fujairah na Ajman.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi huo leo Septemba 26, 2025 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Gulf job Hunts Mohamed Kashif amesem Kampuni hiyo ni Wakala wa Ajira aliyesajiliwa kisheria na Wakala wa Ajira Tanzania (TAESA) chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu.

Kwamba Gulf Jobs Hunts ni tawi la Kampuni ya GULF JOBS HUNTS GROUP yenye Makao Makuu yake Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

"Gulf Jobs Hunts Tanzania inatoa fursa za nafasi za ajira mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usafi, Udereva magari makubwa na madogo, pamoja na Wasaidizi Mizigo Viwanja vya Ndege katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu, Dubai, Abudhabi, Sharjah na Alain," amesema Kashif.

Kwa upande wake Meneja wa Gulf Job hunts manpower Tanzania Shamim Mohamed ametumia fursa hiyo kutangaza nafasi za ajira 5,000 Kwa Madereva wa taksi katika nchi hizo za kiarabu ambapo usaili utafanyika katika ofisi hizo kuanzia Oktoba 6 mpaka 7 mwaka huu.

"Baada ya usaili huu, madereva wataofanikiwa watapewa fursa hizi, Visa ya ajira miaka 2, Leseni ya Udereva ya UAE, nyumba, usafiri wa kazini, Bima ya Afya na likizo moja kwa mwaka," amesema Shamim. 

Naye mwakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Zainab Suleiman ameipongeza kampuni hiyo kwa kuanza kutoa huduma zake nchini na kuunga mkono Serikali katika kutatua na kukabiliana na changamoto za ajira hususan kwa vijana.

Comments