Skip to main content

MBETO AMUUMBUA JUSSA BEI YA KARAFUU ZBAR

 

MBETO AMUUMBUA JUSSA BEI YA KARAFUU ZBAR


Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi  kimemkanya  Makamu Mwenyekiti wa ACT  Wazalendo Zanzibar ,  Ismail  Jussa Ladhu, na kumtaka aache   Siasa za Uongo na Uzushi kwasababu haziwezi kukipatia  hadhi na heshima chama chake .

Katibu wa Kamati  Maalum ya NEC  Zanzibar, Idara ya Itikadi , Uenezi  na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis  amwakanusha uongo  wa Jussa   katika Mkutano  wa  Uzinduzi  wa Kampeni  Jimbo la Fuoni Mkoa Mjini Magharibi kisiwani Unguja. 

Mbeto alisema Viongozi  wa ACT mara zote  wamekuwa wakishindwa kutofautisha kati ya  hatari ya  Uongo  katika  Siasa na   ukweli na uwazi  unaoambatana na dhana  ya  Siasa safi na uongozi bora.

Alisema madai ya Jussa si kwamba yamekivua nguo chama  chake lakini pia yanaendelea kumpunguzia heshima yake  mbele ya jamii  na kumfedhehesha na  kuonekana  ni Mwanasiasa kituko.

"Bei ya Karafuu ilipanda katika  utawala wa Rais Mstaafu Dk Ali Mohamed  Shein  kutoka Shilingi  3000  hadi kufikia  Shilingi 14000 kwa Kilo moja," Alisema Mbeto.

Katibu huyo  Mwenezi  akiusuta uongo  wa  Jusaa , alisema  bei ya karafuu ilipanda tena Dk shein akiwa madarakani  ili ilingane na soko  la dunia  na kufikia   shilingi 21000, hadi  sasa bei  ya karafuu ni shilingi  13000 kwa kilo.

"Mwambieni kibaraka Ian  Smith  wa Zanzibar  apunguze  chumvi ya uongo wake  .Uongo na Uzushi unampunguzia uaminifu na  heshima kwa  Wananchi .Amekuwa Mwanasiasa comedi mwenye  vibweka,"  Alisisitiza.

Mbeto aliitaja Serikali  ya Rais  Mstaafu  Shein ndio iliopandisha bei ya karafuu,   hivyo Jussa anodai  bei   ilipandishwa na Hayati  Maalim Seif Sharif Hamad  ,huo ni  aina mpya ya uongo akimzulia Marehemu. 

Aidha ,alisema   kabla na baada ya Mapinduzi  Mashamba  ya Karafuu kisiwani Pemba,  Serikali iliwakodisha Wakulima  wa   karafuu  jambo ambalo  Serikali ya Rais Dk Mwinyi ilipoingia madarakani ,mashamba hayo sasa yanamilikiwa na  Wakulima   .

Vile vile , madai ya Jussa kuwa ununuzi  wa karafuu hufanywa na kampuni  moja si kweli   utaratibu  ni kwamba  kunakuwa na  ushindani wa  zabuni , kampuni  yenye  bei ya juu hununua  karafuu kupitia  ZSTC  .


Mbeto  alizitaja Kampuni  zilizonunua  Karafuu  ya Zanzibar  ni  Unit Trader  ya India ,  Afcom Trading ya Dubai ,  Brookes Ltd  ,KK Global  Zenj Spice ,   Rkk  ya India na  Rho Traders  African Afrika Kusini   kinyume na madai  ya  Jussa aliiyedai  karafuu  ya    huuziwa  mtu  mmoja .

" Kampuni  tofauti  toka  nchi  tofauti  hununua  Karafuu  ya  Zanzibar  kupitia  Shirika la SMZ la ZSTC  .Kampuni  yenye   bei  kubwa  ndio  inayopewa ruksa na Serikali inunue karafu  Zanzibar " Alisema  Mbeto.

Comments