WANANCHI WA BABATI WAMSHUKURU DKT. SAMIA KWA KUWAFUNGULIA BARABARA
WANANCHI WA BABATI WAMSHUKURU DKT. SAMIA KWA KUWAFUNGULIA BARABARA Babati, Manyara Wananchi wa Kata ya Babati wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa madaraja saba (7) pamoja na kufungua barabara katika kata hiyo ambapo kwa kipindi kirefu wamekuwa wakipata adha ya usafiri hususan kipindi cha mvua. Akitoa pongeze hizo Diwani wa kata ya Babati Mhe. Haruni Msalu amesema kwamba wanamshukuru Rais kwa kuwatendea haki Kata ya Babati kwani Kata hiyo ilikuwa na makorongo mengi sana na kusababisha wananchi kuteseka hasa kipindi cha mvua na hivyo kusababisha kusimamisha kwa muda shughuli zao za kila siku. Amesema katika kipindi cha Awamu ya sita Serikali kupitia TARURA imeweza kujenga madaraja yapatayo saba katika Kata ya babati katika eneo la Amboni C, Kambi ya Fisi, Hostel ya chuo cha uhasibu na Old Majengo-Angoni. “Old Majengo kuja Angoni kulikuwa na kortongo kubwa ambalo lilikuwa likipitisha maji kwenda ziwani, wananchi wakiwemo wanafun