Benk ya NMB yakabidhi Jengo maalumu la kupumzikia wagonjwa wa nje na wasaidizi wao


Mkurugenzi wa NMB na mkurugenzi wa JKCI wakikata utepe kwa pamoja kuzindua jengo hilo







Benk ya NMB  yakabidhi Jengo maalumu la kupumzikia wagonjwa wa nje na wasaidizi wao wanaowaleta wagonjwa kupata huduma katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ililopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.


Akizungumza jana wakati halfa fupi ya kukabidhi  jengo hilo ambalo limegharimu kiasi cha shilingi milioni 30 Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Bi. Ineke Bussemaker alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo lenye uwezo wa kuhifadhi watu 100 kwa pamoja wakiwa wamekaa kusubiri kupata huduma  ni sehemu ni harakati za benki hiyo katika kurejesha kwa  jamii huduma zinazoilenga sekta ya afya ambapo benki hiyo imeweka utaratibu wa kusaidia.


Alisema kukamilika kwa jengo hilo la kupumzikia kutasaidia wagonjwa wa nje na ndugu zao ambao hufika kupata huduma JKCI kupumzika sehemu tulivu na salama huku wakisubiri kuhudumiwa na madaktari wa taasisi hiyo  bila kero
na kuongeza kuwa msaada huo NMB inaamini imeutoa kwa wateja wao pia ambao nao hufika na kupata huduma katika hospital ya muhimbili hususan taasisi ta moyo ta Jakaya Kikwete.

 "Benki ya NMB kwa mwaka 2017 tumejipanga kutumia zaidi ya shilingi bilioni moja kusaidia huduma za kijamii hususani katika sekta ya afya, elimu pamoja na kusaidia majanga mengine yanayoikumba jamii na Kwa mwaka 2016 benki yetu ilitumia takribani milioni 260 nchi nzima kusaidia vifaa mbalimbali vya hospitalini huku jumla ya hospitali 33 zikinufaika kwa msaada huo"amesema Bi BASSEMAKER


Mkurugenzi wa NMB Bi Ineke Bussemaker

Mkurugenzi wa NMB aliyekaa kushoto Bi Ineke Bussemaker akiwa na mkurugenzi wa JKCI Prf Mohammed Janabi


 Kwaupande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Prof. Mohamed Janabi aliishukuru Benki ya NMB kwa msaada huo na na kuongeza kuwa sio mara ya kwanza kwa benki hiyo kuisaidia JKCI katika
shughuli zake. Sambamba na kuishukuru benki hiyo kutoa  msaada huo  mkubwa ambao utawasaidia ndugu ambao huwa wanakwenda kuwatazama wagonjwa wao waliolazwa na kupata matibabu katika taasisi hiyo pamoja na watu wanaokwenda kwa ajili ya kupata matibabu na bata wale wagonjwa wa nje.

Comments