DKT GHARIB BILAL MGENI RASMI UZINDUZI WA KAMPENI YA KILI CHALLENGE CHINI YA GGM NA TACAIDS

KAMPENI YA KILI CHALLENGE KUZINDULIWA LEO DAR ES SALAAM
Picha Mkurugenzi mtendaji Dkt Leonard Maboko (aliyekaa kushoto,Makamo wa rais na miradi endelevu endelevu GGM Bw Simon Shayo (aliyekaa katikati)na msanii Mrisho mpoto ambaye in balozi wa kampeni ya kili Challenge aliyekaa (kulia)

Na Thadei Praygod
Dar es salam

Wito umetolewa kwa wadau Mbali mbali kushirikiana katika mapambano dhidi ya maambukuzi ya ugonjwa wa ukimwi kwa kuungana kwa pamoja katika kampeni ya kili challenge kuhakikisha maambukizi ya ugonjwa huo hayaendelei hapa nchini.

Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na makamo wa rais na miradi endelevu wa mgodi wa dhahabu wa geita (GGM) Bw SIMON SHAYO alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa kampeni ya kili challenge kwa mwaka 2017 unaotarajia kuzinduliwa Leo jioni jijini Dar es salaam.

Bw  SHAYO amesema kuwa kampeni hiyo inayozinduliwa lep inalenga kukusanya fedha kwa ajili ya kutunisha mfuko wa mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI ambayo hufanyika kila mwaka kwa wadau mbali mbali kupanda mlima Kilimanjaro na kuendesha baiskeli kuzunguka mlima huo.
  "changamoto za kijamii ni changamoto za sekta binafsi pia ndiyo maana  Geita Gold Mine (GGM) tumeamua kushirikiana na tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania (TACAIDS) katika mapambano hayo kwa takribani miaka 16 sasa"amesema Bw. SHAYO

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt LEONARD MABOKO ameishukuru kampuni ya (GGM) kwa harakati zake dhidi ya VVU na Ukimwi huku akiongeza kuwa mapambano dhidi yake siyo ya mtu mmoja mmoja Bali ni ya watanzania wote na sekta mbali mbali zikiungana kwa pamoja hatua hiyo itachangia maambukizi ya Ukimwi kupungua mpaka kufikia asilimia 0.3 mwaka 2030 huku akiitaja mikoa ya Njombe,Iringa na Mbeya kama vinara wa maambukizi ya VVU.

Kampeni hiyo ya kili challenge inatarajia kuzinduliwa Leo katika hoteli ya HYATT REGENCY Kilimanjaro  jijini Dar es salaam ambapo mgeni raami anatarajiwa kuwa ni makamo wa rais mstaafu wa serikali ya awamu ya tano Dkt MOHAMMED GHARIB BILAL ambapo hadi sasa zaidi ya watu 700  ulimwenguni kote wameshiriki kuupanda mlima Kilimanjaro na zaidi ya shilingi milioni 800 hukusanywa kwa ajili ya kampeni hiyo ya hisani kila mwaka.

Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo

Comments