Mtu mmoja amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya katani wilayani nyamagana.

Mtu mmoja amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya katani wilayani nyamagana.


Habari ni Kwamba tarehe 23.04.2017 majira ya 18:45hrs jioni katika mtaa wa mkuyuni sokoni kata ya mkuyuni wilaya ya nyamagana jiji na mkoa wa mwanza, mtu mmoja mwanamume aliyrfahamika kwa jina la faraja anselem miaka 31, mkazi wa mtaa wa mkuyuni sokoni, alikutwa akiwa amejinyonga chumbani kwake hadi kufariki dunia kwa kutumia kamba ya katani aliyokua ameifunga kwenye paa la chumba, kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Inasemekana kuwa taraehe tajwa hapo juu marehemu alibaki mwenyewe nyumbani, aidha inadaiwa kuwa kabla ya kufanya tukio hilo marehemu alionekana akiingia chumbani kwake kisha akafunga mlango ndipo baada ya muda kupita watoto waliokua wakicheza maeneo hayo waliona miguu ikining’inia dirishani ndipo walitoa taarifa kwa wazazi wao.

Majirani baada ya kuona tukio hilo walitoa taarifa polisi, ambapo askari walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kuukuta mwili wa marehemu ukining’inia mahali hapo, mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya bugando kwa ajili ya uchunguzi pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi. Aidha upelezi kuhusiana na kifo hicho bado unaendelea.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishina wa polisi ahmed msangi anatoa wito kwa wakazi wa jiji na mkoa wa mwanza, akiwaomba kuwa pale watakapoona mtu amekuwa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu hadi inapelekea kuweza kufanya kitu kisicho cha kawaida cha kuweza kujidhuru yeye mwenyewe au watu wengine, wamfikishe kwa wataalamu wa ushauri nasaha ili waweze kumshauri na kumwaondoa katika hali hiyo ya msongo wa mawazo na kisha kurudi katika hali ya kawaida na kuweza kuendelea na maisha.

Comments