SAKATA LA KUPOTEA KWA BEN SAANANE (UTG) WATOA NENO

Umoja wa kizazi  cha kuhoji Tanzania (UTG)umeliomba jeshi la polisi kutangaza operesheni maalum ya kukomesha vitendo vya utekaji,upoteaji na mauaji ya raia nchini sambamba na kutoa taarifa ya mwenendo wa uchunguzi katika suala la Kupotea kwa BEN SAANANE.

Hayo yamesemwa leo jijini.Dar es salaam na mwenyekiti wa taasisi ya UTG GODLISTEN MALISA   alipokuwa akizungumza na vyombo  vya habari ikiwa ni mwendelezo wa harakati za umoja huo kushinikiza kupatikana kwa katibu mkuu wa taasisi hiyo  BEN SAANANE ambaye alipotea katika mazingira ya kutatanisha tangu mwezi november mwaka jana ambaye mpaka  sasa haijulikani alipo.

Akizungumzia suala la kupotea kwa BEN SAANANE,Bw MALISA amesema kuwa  suala la kupotea kwa BEN ni moja ya matukio ya kupotea kwa watanzania mbali mbali yaliyoripotiwa siku za karibuni huku baadhi ya matukio hayo yakiogofya kutokana na kuambatana kwa vitendo vya utekaji/utesaji na hata kifo.

Aidha ameongeza kuwa kutokana na vitendo hivyo,UTG imechukua hatua mbali mbali ikiwemo kuwasilisha malalamiko rasmi (ya maandishi)kwa tume ya haki za binadamu.na utawala bora  ambayo kikatiba ina.mamlaka ya kusikiliza mashauri yanayohusu ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala bora.
"Pia UTG imekiomba kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kupeleka.malalamiko rasmi umoja wa mataifa (UN) juu ya matukio ya watanzania kupotea na ikumbukwe kuwa mapema mwezi uliopita mkurugenzi wa LHRC Dkt HELEN KIJO BISIMBA alishiriki mkutano wa umoja wa mataifa wa taasisi za kiraia zinazoshughulika na masuala ya haki za binadamu ambapo aliweza kupenyeza hoja ya kupotea kwa watanzania katika mazingira ya kutatanisha akihusisha na suala la kupotea kwa ben saanane na baada ya kuwasilisha hoja hiyo umoja wa mataifa ulimtaka Dkt KIJO kuwasilisha kwa njia ya maandishi malalamiko hayo ili umoja wa mataifa utume wataalam waje kuchunguza hivyo tulishirikiana na LHRC kuhakikisha kuwa barua ya malalamiko hayo inaaandikwa na kufika katika umoja huo katika taratibu rasmi na tayari barua hiyo imeshatumwa na tunasubiri.majibu"amesema Bw MALISA

Hata hivyo katika hatua nyingine UTG)umeliomba bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kujadili hoja kuhusu kudorora hali ya usalama ya usalama nchini kufuatia matukio ya kupotea,kutekwa na kuuawa kwa baadhi ya watanzania katika.maeneo mbali mbali nchini huku ikitoa pole kwa jeshi la polisi na familia za askari 8 waliopoteza maisha wilayani Kibiti mkoani Pwani baada ya kushambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi..



Comments