"TAASISI ZA SERIKALI ZILIPE BILI ZA MAJI"Prof KITILA MKUMBO

       Pich,mtendaji mkuu wa DAWASCO mhandisi Cyprian Luhemeja aliyesimama kulia akitoa taarifa ya huduma za maji kea mikoa ya Dar na pwani kwa Prof Kitila mkumbo aliyekaa kushoto.



DAR ES SALAAM.
April 18,2017

Katibu mkuu wa wizara ya maji na umwagiliaji Profesa KITILA MKUMBO amelitaka shirika la maji safi na maji taka Dar es salaam (DAWASCO) pamoja na mamlaka ya maji safi.na maji taka jijini hapa (DAWASA)kuhakikisha wanatatua changamoto za upatikanaji wa maji kwa kuwekeza zaidi katika usambazaji wa maji ili wananchi wanufaike kiurahisi na huduma hiyo.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam wakati katibu mkuu huyo alipofanya ziara yake ya kwanza ya kikazi katika shirika la (DAWASCO) na kuzungumza na bodi ya wakurugenzi na mameneja wa mashirika hayo (DAWASCO,DAWASA)huku akiongeza kuwa mkoa wa Dar es salaam una uhitaji mkubwa wa maji hivyo kama mashirika hayo yatafanya jitihada kubwa ikiwemo kuboresha miundombinu  ya maji kabla ya mwaka 2020 yatazalisha  zaidi ya lita milioni milioni 500 kwa siku  ambayo ndo mahitaji ya mkoa huo

Aidha ameyataka mashirika hayo kuhakikisha mikoa ambayo inahudumiwa na.mashirika hayo mawili inapata huduma ya maji kwa kuhakikisha mashirika binafsi na ya serikali yanayopata huduma za maji kulipia bili zao kwa wakati kwani kutolipa bili za maji kwa wakati kunachelewesha  huduma ya maji kuwafikia wananchi wengi zaidi kutokana na.mashirika hayo kukosa fedha za kuboresha miundombinu ya maji.

"kama mwananchi wa kawaida tena wa kipato cha chini analipa bili za maji kwa wakati kwa nini taasisi kubwa tena za serikali ambazo hupewa pesa zishindwe kulipa.?"amesema Profesa KITILA.

Kwa upande wake afisa mtendaji mkuu wa shirika la.maji safi na maji taka Dar es salaam (DAWASCO)mhandisi CYPRIAN LUHEMEJA amesema changamoto kubwa shirika hilo linalokabiliana nazo ni pamoja na upotevu mkubwa wa maji  unatokana na uchakavu wa miundo mbinu ya maji ikiwemo mabomba ya kusafirishia maji hayo kwenda kwa watumiaji pamoja na wizi wa maji unaofanywa na baadhi ya wananchi wasio waaminifu na wamefanya jitihada mbali ikiwemo uboreshaji ili  kuhakikisha upotevu huo wa maji unapungua na hatimaye kumalizika kabisa ambapo kwa sasa umepungua kutoka asilimia 57 mwaka 2015 na kufikia asilimia 37.8 mwezi march mwaka huu.




Picha,katibu mkuu wizara ya maji na Prof Kitila Mkumbo wa kwanza kushoto akionyesha kufurahia jambo na wenyeji wake afisa mtendaji mkuu (DAWASA)Mhandisi Archard Mutalemwa (katikati)pamoja na afisa mtendaji mkuu (DAWASCO)mhandisi Cyprian Luhemeja wa kwanza kulia katika makao makuu ya DAWASCO









Comments