TRL YAZINDUA TRENI YA KUSAFIRISHA MIZIGO DAR,DODOMA

 

Shirika la reli Tanzania (TRL) Leo Limeanzisha safari  ya  treni ya mizingo (FLAG OFF) ya  shirika la  mpango wa chakula duniani (WFP) lenye  lengo  la kuhudumia  wateja kwa kiasi  na muda  unaoridhisha  na kufikisha bidhaa kwa walaji wake.




Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mapema Leo jijini dar es salaam mkurugenzi mtendaji wa TRA Masanja Kadogosa  amesema kuwa kihistolia huduma hii ilikuwepo  tokea enzi za shirika la reli  Tanzania  TRC na  katika mwaka  2004 ilikuwa imeshasafirisha  jumla ya tani 400,723 za WFP na kuanzia  mwaka  2006 ukashuka tokea  tani  66,994 hadi tani  846  tu mnamo mwaka 2015.



Aidha amesema kuwa moja kati ya changamoto iliyopo  ni ukosefu wa vichwa vya Tren vya kutosha na mabehewa Hata hivyo  baada ya kujipanga na kuihakikishia huduma zinakamirika kusafirishia tani  7000 za mahindi kupeleka katika ghala kuu la WFP iliyoko  Kiota  Dodoma .




Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya TRL John Kondoro amesema kuwa tangu mwaka 2000 hii ni Mara ya pili shirika hilo linasafirisha mizigo na kwa sasa wamesafirisha mzigo mkubwa na hii ikiwa ni faida maana inaongeza faida kwa shirika na kwa kufika hatua hiyo imani kubwa inajengeka kwa wadau kwa kazi hii inayofanyaka.

Comments