UHALIFU WA "KWA MROMBOO",USWAHILINI NA MAENEO JIRANI SASA KUMALIZIKA ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo ameweka Jiwe la Msingi kwenye Kituo cha Polisi Kata ya Muriet wakati wa ziara ya Kikazi Jijini hapa yenye lengo la kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kutatua kero za wananchi.
Akiweka jiwe la Msingi Mhe. Gambo amesema kwa muda mrefu alikua anakerwa na uhalifu uliokithiri katika eneo hilo na hali hiyo kumsukuma yeye kutafuta mfadhili kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa kituo cha Polisi kitakachosaidia kudhibiti masuala ya Uhalifu.
Aliongeza kuwa baada ya kumpata mfadhili huyo alimlete eneo la ujenzi ambapo pia wahalifu walimuibia Simu yake mbele ya viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ndipo na mfadhili alipopata ari ya kuanza ujenzi huu haraka iwezekanavyo.
“Haiwezekani mtu anaiba mbele ya Kamanda wa Polisi hakika hii ilituthibitishia kwamba uhalifu katika eneo hili umekithiri na kwa sababu hakunha Kituo cha Polisi wahalifu wanapata mwanya wa kufanya kazi hii isiyo halali kwa ujasiri zaidi” Alisema Gambo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mfadhili ambaye ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Lodhia Ndg. Haruni alisema amejitolea sehemu ya mali zake ili kuwasaidia Watanzania wenzake wanaoteseka na tabia za uhalifu zinazorudisha nyuma maendeleo
Ujenzi wa Kituo hicho utakaogharimu zaidia ya Tsh Mil 200 utakamilika mnamo mwezi Juni 2017.
Mkuu wa mkoa wa Arusha MRISHO GAMBO akisalimiana na wakazi wa kata ya Muriet |

Mkuu wa mkoa wa Arusha mrisho Gambo Kushoto akifurahia jambo baada ya kuzindua ujenzi wa kituo hicho cha muriet |
Comments