WASAFI VS SHIGONGO HAPATOSHI

kuna msemo wanasemaga ukimwaga mboga namwaga ugali,msemo huu ni maarufu sana hapa nchini hasa kwa waswahili.

Hiyo inaweza kuwa maana halisi ya hali iliyoibuka katika mitandao ya kijamii kati ya mashabiki wa msanii harmorapa na wale wa WCB inayoongozwa na CEO,Diamondplatnums baada ya mfanyabiashara na CEO wa Global Publisher Erick Shigongo kuandaa show ambayo itamtambulisha msanii harmorapa pande za mbagala DAR LIVE ambayo inafanyika leo huku kiingilio kikiwa ni buku tano,sasa masaa machache kabla ya kufanyika kwa show hyo timu ya wasafi yaan Rich Mavoko na Harmonize nao wameandaa show yao mita chache tu kutoka pale inapofanyika show ya harmorapa tena ya kwao ikiwa ni bure kabisa yaan isiyo na kiingilio.

Sasa hali hyo imepelekea watu wengi kumlaumu mwanamuziki #diamond kuwa anataka kumkomesha hasimu wake #erick shigongo ambaye juzi kati waliingia katika sintoelewana baada ya mfanyabiashara huyo kumtuhumu.msanii huyo kwa mambo kadhaa ikiwemo kufanya.show za bei ghali ndani ya nchi yake huku wengine wakionyesha kufurahia jambo hilo.

Siyo kwamba tunasema kuwa wasafi imeandaa show ili kumkomoa erick shigongo na harmorapa lah bali hizo nu hisia za baadhi ya mashabiki ambazo wamezionyesha wazi wazi kufuatia WCB

kutangaza kufanya show ya bure katika eneo hilo hilo ambalo harmorapa atafanya show yake DAR LIVE (pembezoni tu mwa uwanja wa mbagala zakheem).

Comments