DUKA KUBWA LA MANUNUZI YA VIFAA VYA UJENZI (BUILDER'S CENTER) LAFUNGULIWA NA WACHINA DAR ES SALAAM.

DUKA KUBWA LA VIFAA VYA UJENZI (BUILDER'S CENTER) LAFUNGULIWA NA WACHINA DAR ES
SALAAM.



Awali akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa duka hilo linaloendeshwa na kampuni ya kimataifa ya CHINA NATIONAL BUILDING MATERIAL GROUP LIMITED (CNBM) waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji. Charles Mwijage   ameipongeza kampuni hiyo na  kuongeza kuwa  kuwa kampuni hiyo imejenga zaidi ya asilimia 65 ya viwanda vyote vya saruji na vioo  duniani.

Waziri Mwijage amesema kuwa kampuni ya CNBM ina uwezo mkubwa katika uzalishaji wa saruji  na imekuwa ikizalisha tani 530 milioni kwa mwaka wakati uwezo wa Tanzania katika viwanda vilivyosimikwa ni tani milioni 10.8 na kubainisha kuwa kiasi kinachohitajika nchini ni tani milioni 4.8.

Ameongeza kuwa CNBM inatarajiwa kushirikiana na mwekezaji mwingine ambaye anakwenda kujenga kiwanda Tanga kitakachozalisha  tani milioni saba za saruji na kubainisha kuwa hakuna kiwanda kinachozalisha tani milioni saba Tanzania.

   “Hawa wenzetu hawakimbilii kutafuta vifaa vya ujenzi  kutoka nje bali wanatambua wawekezaji wa Tanzania,viwanda vya tanzania wanafanya navyo wana wataalamu wanawaelekeza wazalishe kwa viwango anavyovihitaji vya kimataifa na tumeona humu kuna nyaya”, alisema Mwijage

Waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji,Charles Mwijage




Nae Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lv Youqing amesema kuwa urafiki baina ya  China  Tanzania ni wa kihistoria tangu kwa Rais Xi Jinping ambapo urafiki huo umekuwa  wa mwendelezo hadi kwa serikali ya  awamu ya tano ya Rais John Magufuli.


Balozi wa China hapa nchini Lv Youqing





Aidha Mkurugenzi wa Builder's Center Tanzania Bw. Andy Chen amesema kampuni hiyo ya (CNMB) inatoa fursa ya kazi kwa watanzania pamoja na kutoa mafunzo yatakayowasaidia kuendana na sera ya Tanzania ya viwanda.

Mkurugenzi wa Builder's Center Tanzania,Andy Chen





"Tutaendelea kujenga maduka mengine Tanzania kulingana na ukuaji mkubwa wa uchumi wa Tanzania na ukuaji wa soko la ndani" amesema bwana CHEN

Comments