IRENE UWOYA AWA BALOZI WA KAMPUNI YA SIMU YA ITEL MOBILE TANZANIA











#ITELMOBILETANZANIA YAMTAMBULISHA IRENE UWOYA KAMA  BALOZI WA KAMPUNI HIYO "BRAND AMBASSADOR" TANZANIA

Kampuni ya simu ya Itel Tanzania Leo kwa Mara ya kwanza jijini Dar es salaam imemtambulisha balozi wa kampuni hiyo hapa nchini ambaye ni msanii kutoka bongo movie IRENE UWOYA

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumtambulisha na kutiliana saini ya makubaliano na balozi huyo meneja masoko wa kampuni hiyo WOLLE FERNANDO amesema kampuni hiyo imeingia mkataba wa mwaka mmoja na msanii huyo ambaye watashirikiana naye katika kutoa elimu kuhusu bidhaa za Itel hasa kwenye matukio ya ukarimu kwa baadhi ya makundi ya jamii yaan (charity event programs) .

Kwa upande wake balozi huyo IRENE UWOYA ameishuukuru kampuni hiyo kwa kumchagua yeye kama balozi huku akiahidi kushirikiana na kampuni hiyo kwa hali na Mali kama (brand Ambassador) katika kuitangaza kampuni hiyo sambamba na kushiriki katika masuala ya kijamii yatakayoihusisha Itel mobile Tanzania.

Kampuni hiyo ya Itel mobile Tanzania ambayo makao yake makuu yako jijini Dar es salaam kwa nchi ya Tanzania ilianza kufanya kazi hapa nchini tangu mwaka 2007 ambapo kwa mwaka huu inatimiza miaka 10 tangu kuanza kuuza bidhaa zake hapa nchini.


Comments