Jambazi "MREMBO ZAIDI"azikwa baada ya kuuawa na polisi

Jambazi "MREMBO ZAIDI"azikwa baada ya kuuawa na polisi

Picha ya mrembo huyo enzi za uhai wake




-Mwizi wa kimabavu wa kike aliyepigwa risasi katika eneo la Kayole nchini kenya amezikwa Murang’a

Cleah Addi Vybz kwa jina kamili Clare Njoki alikuwa na umri wa miaka 17 pekee alipouwawa

Njoki aliacha shule akiwa katika kidato cha kiwanza na kuelekea Kayole, Nairobi Cleah Addi Vybz kwa jina halisi Clare Njoki ametajwa na wengi kama jambazi mrembo zaidi nchini Kenya.
 Njoki aliuwawa na polisi katika eneo la Kayole mnamo Jumanne, Mei 9. Sasa maelezo mapya yameibuka kuhusu mhalifu huyo.  Msichana huyo anatoka kijiji cha Kambirwa, eneo bunge la Kiharu katika kaunti ya Murang’a.




Njoki alizikwa mnamo Alhamisi, Mei 18 katika mazishi yaliyohudhuriwa na idadi ndogo ya watu. TUKO.co.ke imepekua na kugundua Claire aliishi na bibi yake katika eneo la Kambirwa kabla ya kuacha masomo akiwa kidato cha kwanza katika shule ya upili ya Gikindu Secondary School na Baadaye Njoki alielekea kuishi na mamake katika eneo la Kayole, Nairobi. Inasemakana alikutana na watu waliomuingiza katika uhalifu. Habari za kifo cha Njoki ziliwashangaza watu wa familia yake, marafiki na waliosoma naye ambao hawakujua maisha yake ya uhalifu.
 Baadhi yao walitilia shaka ripoti ya polisi kuwa alikuwa jambazi sugu. Aidha, watu wa familia ya Njoki walidai hakuwa na mtoto wala hakuwa ameolewa.  Shule alikosomea Clare Njoki. Machapisho yake ya awali katika Facebook yalionyesha picha ya mtoto huku polisi wakisema mumewe Njoki alikuwa mhalifu.



Picha ya Kaburi lamrembo huyo

Comments