JAY Z AMPIGA "goli LA mkono"DR DREE

JAY Z AMPIGA "goli LA mkono"DR DREE forbes
Baada ya kuwaona wasanii kutoka Afrika ambao wanaongoza kuwa na mitonyo katika Forbes Afrika, lets move on mpaka mamtoni ambapo tunakutana na wasanii wa HipHop ambao mitonyo yao sio ya mchezomchezo.
Kupitia jarida la Forbes limetoa orodha ya wasanii wa HipHop ambao ni matajiri zaidi duniani, orodha hiyo imetolewa kwa mwaka huu ambapo tunakutana na Diddykama kawaida anashikilia nafasi yake ya kwanza na hiyo ni kutokana na endorsement ya  Diego’s Ciroc, alkaline water Aquahydrate na DeLeon tequila wote hawa wakimsogeza mpaka kwenye mtonyo wa  $820 million.
Jay z amefanikiwa kumpiku Dre na kuwa nafasi ya pili ya wasanii wa HipHop matajiri zaidi Duniani baada ya kuingia dili na mtandao wa Sprint ambao ameinvest takribani $200 million, na inasemekana analipwa mara 10 zaidi ya mara kwanza, Bird Man akiwa nafasi ya nne ndani ya listi hiyo huku Drake akiwa kwenye nafasi ya tano.
                                                        1. Diddy $820m = TZS 1.8tr
  
2. Jay Z $810m = TZS 1.8tr
  3. Dr Dre $740m = TZS 1.7tr
  4. Birdman $110M = TZS 245bn
 
5. Drake $90M = TZS 201bn
    

Comments