MIFUKO YA PICS 'KINGA NJAA' YA KUHIFADHIA MAZAO BILA DAWA YAWA MKOMBOZI KWA WATANZANIA, WASISITIZWA KUITUMIA.
MIFUKO YA PICS 'KINGA NJAA' YA KUHIFADHIA MAZAO BILA DAWA YAWA MKOMBOZI KWA WATANZANIA, WASISITIZWA KUITUMIA.
![]() |
Mshauri mwelekezi wa mifuko ya Pics maarufu kama Kinga njaa inayotengenezwa na kiwanda Cha Pee Pee Tanzania Ltd Cha Mkoani Tanga ,Bi Bernadette Majebele akiwaonyesha wanahabari waliotembelea Banda lao katika maonyesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania mfuko wa Pics ambao inatumika kuhifadhia mazao ya nafaka bila dawa. |

![]() |
Sehemu ya bidhaa za nyuzi zinazotengenezwa hapa nchini na kiwanda Cha PPTL Kilichopo Kange Mkoani Tanga zikiwa Katika banda la kiwanda hicho katika maonyesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yanayofanyika katika uwanja wa kimataifa wa maonesho ya biashara sabasaba kuanzia desembar 3 Hadi 9 mwaka huu Jijini Dar es salaam. |
![]() |
Mshauri mwelekezi wa mifuko ya Pics maarufu kama Kinga njaa inayotengenezwa na kiwanda Cha Pee Pee Tanzania Ltd Cha Mkoani Tanga ,Bi Bernadette Majebele akiwaonyesha wanahabari waliotembelea Banda lao katika maonyesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania mfuko wa Pics ambao inatumika kuhifadhia mazao ya nafaka bila dawa. |
Na Thadei PrayGod, Dar es salaam.
Wito umetolewa Jijini Dar es salaam na mshauri mwelekezi wa mifuko hiyo Bi Benadette Majebele alipokuwa Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea Banda la kiwanda cha PPTL katika maonyesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yanayofanyika katika uwanja wa kimataifa wa maonesho ya biashara (sabasaba)kuanzia desembar 3 Hadi 9,2022.
Bi Bernadette alisema kuwa mifuko hiyo imetengenezwa ikiwa na Tabaka tatu, na inatumika kuhifadhia nataka kavu bila kuongeza dawa au kemikali ya aina yoyote ile.
" kama mnavyoona waandishi hapa tuna maturubai ambayo yanatumika kukaushia mazao lakini kibwa ZAIDI ni mifuko ya Kinga njaa ambayo imetengenezwa maalum Kwa ajili ya kuhifadhia mazao bila kutumia dawa Kwa sababu changamoto iliyokuwepo ni wadudu kuharibu mazao katika muda mfupi baada ya kuhifadha hasa majira ya joto, mdudu ni kiumbe hai anahitaji hewa, maji na chakula kwa hiyo mazao yakiwekwa katika hii mifuko kutokana na uzito wa zile tabaka mbili za ndani ambazo hazipitishi hewa mdudu anashindwa kuendelea kuishi na hata mayai ambayo Kwa kawaida yanakuwa yako kwenye mazao toka shambani hayawezi kuanguliwa katika mifuko hii ya Pics"alisema Bi Bernadette.
Aliongeza kuwa teknolojia ya utengenezaji wa mifuko hiyo ilianza kuzalishwa hapa Tanzania na kiwanda Cha PPTL Kilichopo Kange,Mkoani Tanga mwaka 2014 na imeendelea kuzalishwa mpaka leo ambapo pia imekuwa ikiuzwa nje ya nchi kama Kenya, Rwanda, Burundi na mwaka huu kiwanda hicho Kimeanza kuiuza katika nchi za Afrika ya Kati.
"mwanzoni mifuko hii ilianza kutumika katika ngazi ya familia lakini Kwa sasa tunahamasisha watanzania kuitumia katika ngazi ya biashara kwani imekuwa mkombozi mkubwa Kwa mazao hasa kipindi hiki ambacho mazao yameongezeka bei hivyo kama wafanyabiashara watatumia mifuko hii wataongeza kipato kwani mazao hayaliwi na wadudu"aliongeza.
Aidha amewasihi watanzania kuacha kutumia dawa Kwa ajili ya kuhifadhia mazao kama mahindi na badala yake watumie mifuko ya Pics 'kinga njaa' ambayo ni mkombozi wa mazao hapa nchini na inajali afya za walaji wa mazao hayo kutokana na mifuko hiyo kutotumia dawa wala kemikali yoyote katika kuhifadhia mazao.
Hata hivyo Bi Bernadette aliwaomba watanzania kutembelea Banda lao katika maonyesho hayo yanayofanyika katika uwanja wa kimataifa wa maonesho ya biashara (sabasaba) Jijini Dar es salaam ili kujionea mifuko hiyo na kupata maelezo juu ya ununuzi wake.
Mifuko ya Pics ilibuniwa baada ya wataalam wa chuo kikuu Cha Purdue nchini Marekani kufanya utafiti na kuamua kuja na nyenzo bora za kuhifadhia mazao ya nafaka ndipo wakabuni teknolojia ya mifuko hiyo iliyoitwa Purdue Influede Crops Storage (Pics) na sasa inatumiwa na baadhi ya wakulima katika baadhi ya nchi barani Afrika na imekuwa mkombozi katika uhifadhi wa kisasa wa mazao bila kutumia dawa.
Comments