JENEZA LA "Jambazi mrembo zaidi"LAPASUKA WAKATI MWILI WAKE UKISHUSHWA KABURINI.

JENEZA LA "Jambazi mrembo zaidi"LAPASUKA WAKATI MWILI WAKE UKISHUSHWA KABURINI.













Kituko kwenye maziko ya marehemu Claire Njoki's mjini Muran'ga nchini Kenya  karibu kutibue shughuli nzima ya maziko ya mrembo huyo ambaye wakenya wengi wanamtaja kama jambazi mrembo zaidi nchini humo

Kituko hicho hakikutokea kwa sababu ya polisi kuvamia na kuwakamata watu, bali kilitokea wakati jeneza likiteremshwa kaburini






 Picha ya mtandaoni inaonesha jeneza lililovunjika mara walipoanza kurusha mchanga kulifunika Tukio la kushangaza lilitokea wakati jeneza la mwili wa jambazi mrembo sana jijini Nairobi lilipokuwa likiteremshwa kaburini Kaunti ya Murang'a. alikuwa sehemu ya kundi hatari la majambazi kwa jina Gaza ambalo limekuwa likiwaangaisha wakazi wa Nairobi kwa muda mrefu.








Claire Njoki Kibia mwenye umri wa miaka 17 alipigwa risasi na kuuawa huko Kayole na Hamna historia ya marehemu iliyosomwa na maziko hayo yalikuwa na upole mwingi na huzuni na yalihudhuriwa na familia na majirani. Marafiki zake hawakuhudhuria maziko hayo labda kwa kuhofia polisi waliovalia kawaida waliokuwa kwenye maziko hayo.





Mpaka hivi sasa tukio la kuuawa jambazi Huyo wa kike limekuwa likizungumzwa sana katika mitandao mbali mbali nchini humo na kuwashangaza watu wengi.


Comments