Maadhimisho ya mazingira yapelekwa kufanyika kwa Nyerere.

Maadhimisho ya mazingira yapelekwa kufanyika kwa Nyerere.

Waziri makamba aliyekaa kulia akiongea na wanahabari (hawapo pichani)




Dar es Salaam.Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), imesema Maadhimisho ya  Siku ya Mazingira Duniani kitaifa itafanyika Butiama mkoani mara ili kumuenzi Mwalimu Julius Nyerere.

Akizungumza na wanahabari leo, waziri wa wizara hiyo, January Makamba amesema Juni 5 kila mwaka Tanzania inaungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya mazingira yaliamuliwa na Baraza la Umoja wa Mataifa la mwaka 1972.

Makamba amesema lengo la kupeleka maadhimisho hayo Butiama ni kumuenzi Nyerere ambaye alikuwa mwanamazingira namba moja nchini sanjari na kukumbuka mchango wake katika masuala ya uhifadhi wa mazingira nchini.

Kwa mujibu wa Makamba ambaye ni Mbunge wa Bumbuli Mkoani Tanga, kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu nchini ni utunzaji wa mazingira na maendeleo ya viwanda.

Comments