MWANAMKE AFARIKI MIEZI MINNE BAADA YA KUTABIRI KIFO CHAKE MTANDAONI.


MWANAMKE AFARIKI MIEZI MINNE BAADA YA KUTABIRI KIFO CHAKE MTANDAONI.
Marehemu Irene Chris akiwa na mumewe Chris Mwangi siku ya harusi yao.
Mara nyingi wa wengi wamekuwa wakitabiri mambo mbali mbali maishani mwao na hata wengine kujikuta wakijitabiria kifo bila kujua.

Irene Chris aliyeolewa kwa harusi kubwa Agosti 2016 na mumewe Chris Mwangi - Mnamo January 2017, Irene aliandika katika mtandao wa kijamii kwamba alikuwa akielekea mbinguni na kuwaomba watu kutuma salamu ili awasaidie kuzifikisha huko mbinguni.
-Miezi minne baadaye, mwanamke huyo mrembo ameaga dunia na marafiki zake wamejua kuwa alikuwa na hisia kwamba angeaga dunia ingawa hakuna yeyote mwenye hakika na hilo.

Irene Chris, mkewe Chris Mwangi alikuwa na maono ya kifo chake. Alidokeza hata katika mitandao ya kijamii ingawa ni wachache waliofahamu.

Wengi marafiki zake walimkosoa kwa kusema hilo na kumwambia kuondoa ujumbe huo pamoja na kukoma kuzungumzia kifo angali yu hai.

 Wengine walipuuzia  mbali ujumbe huo kwa kusema ulikuwa utani lakini Katika ujumbe mwingine, mwanadada huyo alisema alikuwa akikumbuka marafiki zake ambao  walikwishakufa . Lakini hakuna aliyeshikanisha jumbe hizo kwamba alikuwa akiwaaga kwaheri.
Huu ndo ujumbe aliouandika kupitia ukurasa wake wa Facebook miezi minne iliyopita.

Irene alizikwa nyumbani kwa mumewe Wanyororo,Lanet, Kaunti ya Nakuru Alhamisi Mei 25 na kuacha mumewe na mtoto wake wa wiki mbili.

Comments