MWANAMKE ALIYEHARIBIWA SURA NA TINDIKALI AOLEWA INDIA.

MWANAMKE  ALIYEHARIBIWA SURA NA TINDIKALI AOLEWA INDIA.






Katika ulimwengu wa sasa wanawake/wanaume wengi hupenda kupata wenzi wao ambao wana mionekano mizuri na ya kuvutia na inapotokea MTU ameoa au kuolewa na mtu aliyemzidi umri,kipato au bata mwenye sura isiyo ya kawaida katika jamii watu husema kuwa amefuata pesa tu na siyo mapenzi ya kweli



Lakini hali ni tofauti kwa Binti Lalita Ben Bansi, binti wa kihindi ambaye aliharibika sura yake baada ya kumwagiwa tindikali na ndugu yake mwaka 2012 na sura yake kuharibika Mara nyingi watu ambao amekuwa akikutana nao njian wengi humkimbia kutokana na muonekano wa sura yake na bata watoto humwogopa wakutanapo naye.





Lakini amani ya moyo ilirejea tena kwa binti Huyo Mara baada ya kukutana na Ravi Shankar ambaye alimpenda na kuahidi kumuoa na ndoto yake ikakamilika mwezi huu kwa mwanadada Huyo anayeishi jijini Mumbai nchini India kufunga ndoa na Ravi ambaye ni mwanaume aliyetokea kumpenda binti huyo

Comments