MWANAMKE ALIYEMKATAA KUOLEWA NA OBAMA MARA MBILI.
MWANAMKE ALIYEKATAA OMBI LA
KUOLEWA NA OBAMA MARA MBILI
Mara nyingi wanawake au wanaume wengi huwa na tabia ya kukataa kuoa au kuolewa na MTU Fulani kwa sababu Fulani lakini baadaye baadhi yao huyajutia maamuzi waliyofanya.
Kitabu kipya kuhusu maisha ya rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama kinadai kuwa Obama alitoa ombi la ndoa mara mbili kwa mpenzi wake wa zamani, Sheila Miyoshi Jager. Kitabu hicho kipya, Rising Star: The Making of Barack Obama kilichoandikwa na David Garrow kinadai kuwa Obama alitoa ombi hilo mara ya kwanza mwaka 1986 lakini wazazi wa Jager hawakufurahishwa na pendekezo hilo. Wakati huo, Obama alikuwa na umri wa miaka 25 naye Jager akiwa na miaka 23.



Comments