TGNP MTANDAO YAWAPONGEZA WASICHANA WALIOFANYA VIZURI KATIKA VYUO MBALIMBALI NCHINI

TGNP MTANDAO YAWAPONGEZA WASICHANA WALIOFANYA VIZURI KATIKA VYUO MBALIMBALI NCHINI








TGNP Mtandao imesema kuwa changamoto inayowakabili wanafunzi wa vyuo  vikuu nchini ni rushwa ya ngono.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwapongeza wasichana 38  waliofanya vizuri katika elimu ya Juu kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa  TGNP,  Lilian Liundi amesema wanawake wengi wanashindwa kufikia malengo kutokana na changamoto ya ngono na kufanya wanawake kuwa wanyonge.
Amesema kuwa wanawake wanaonekana daraja la pili hali ambayo inafanya kuendelea kuweka mfumo dume wa maamuzi kufanywa na wanaume.Lilian amesema kuwa wasichana ambao wamefanya vizuri  katika vyuo mbalimbali inaonyesha ukombozi wa wanawake katika kuleta maendeleo ya kumuokoa mwanamke mwezie.
Aidha amesema kuwa TGNP Mtandao imekuwa katika mstari wa mbele katika kuendesha harakati za kumkombo mwanamke katika changamoto mbalimbali.Mmoja wahitimu wa waliofanya vizuri , Aisha Soudy  kutoka  Chuo cha  Teku, amesema kuwa wasichana wanachangamoto nyingi ikiwemo na mila na tamaduni ambayo unampendelea zaidi mtoto wa kiume.
Amesema kuwa yuko tayari katika kufanya ukombozi wa mwanamke kwa kutoa msaada pale anapoona anawajibu wa kufanya kwa ajili ya kumuinua Mwanamke.

Kwa upande wa Mhitimu aliyefanya vizuri katika matokeo ya Chuo Kikuu cha Dodoma, Sara Mgonela amesema kuwa msichana ana nafasi yake kama  akijitambua anataka kufanya nini katika jamii yake katika kuleta tofauti  kuliko vile wanavyofikiria.Sara amesema kuwa licha kukabiliwa na changamoto kama mtoto wa kike lakini ameweza kufanya vizuri na kuwataka wasichana kujiamini kuwa wanaweza.

Mkurugenzi mtendaji wa TGNP,Lilian Liundi akizungmza na waandishi habari katika hafla ya kuwapongeza wasichana waliofanya vizuri katika matokeo uliofanyika jana katika Ukumbi wa TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam.






Msichana aliyefanya vizuri katika Chuo Kikuu cha Dodoma, Sara Mgonela akizungmza na waandishi habari juu umahiri wake ambao ulimuwezesha kufanya vizuri katika matokeo ya mwisho katika chuo katika hafla ya kuwapongeza wasichana waliofanya vizuri katika matokeo uliofanyika jana katika Ukumbi wa TGNP Mtandao jijini Dar es Salaam.



 Msichana aliyefanya vizuri katika Chuo Kikuu cha  Kairuki, Flora Njiku akizungmza na waandishi habari juu rushwa ya ngono kwa watoto wa kike vyuoni katika hafla ya kuwapongeza wasichana waliofanya vizuri katika matokeo ya vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini uliofanyika jana katika Ukumbi wa TGNP jijini Dar es Salaam.


Comments