Wapenzi wasiofunga ndoa mpaka disemba 2017 kwenda jela.

Wapenzi Wapenzi wasiofunga ndoa mpaka kufikia disemba 2017 kuchukuliwa hatua kali na serikali.








Serikali ya Burundi ijumaa iliyopita iliwashangaza wananchi wake baada ya  kuwaawaamrisha wapenzi wote nchini humo kuchumbiana na kuona haraka iwezekanavyo kabla  sheria Kali ichukuliwe dhidi yao

Serikali ya nchi hiyo imewapa masharti ya hadi mwisho wa mwaka huu 2017 kuhalalisha mahusiano na ndoa zao kabla ya hatua kali kuchukuliwa na Inasemekana amri hii inanuia kudumisha maadili mema katika jamii na kuzuia ndoa zisizo halali na wasichana wadogo kupachikwa mimba kiholelela.

Amri hiyo ambayo ilitolewa na wizara ya maswala ya ndani ya Burundi Ijumaa Mei 27 kupitia kwa  Msemaji wa wizara hiyo, Terence Ntahiraja alisema kuwa wapenzi wamepewa muda wa miezi saba yaan hadi mwishoni mwa mwaka huu kuhalalisha ndoa zao. 

Aidha inasemekana kuna baadhi ya mashirika yamejitolea kuwasaidia wapenzi ambao hawajiwezi kufunga ndoa zao lakini Raia wa nchi hiyo wamepingana na sheria hiyo kwa kudai kuwa inakiuka misingi ya haki za binadamu lakini serikali ya Burundi imeshikilia msimamo wake kwa kudai kuwa amri  na sheria hiyo pia iko kwenye katiba ya nchi hiyo.

Comments