Je bado watu wanye Ualbino wana hofu juu ya maisha yao?majibu yako hapa

Watu wanaoishi na ualbino katika maeneo ya vijijini  wameendelea kuishi kwa hofu wakiogopa vitendo vya ukatili dhidi yao.






Hayo yamesemwa mbele ya wanahabari wakati wa hitimisho la ziara yake hapa nchini mtaalamu wa kujitegemea kuhusu kunufaika na haki za binadamu kwa watu wenye ualbino aliyeteuliwa na baraza la umoja wa mataifa linaloshughulikia haki za binadamu Bi IKPONWOSA ERO.

Bi Ero amesema kuwa ingawa mashambulizi yaliyoripotiwa dhidi ya watu wenye ualbino yamepungua lakini bado watu wenye ualbino katika maeneo ya vijijini wanahofia usalama wao.

Aidha Bi Ero amesisitiza kuhusu wasiwasi kuhusu shule zinazotumika kama vituo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya watoto wenye ualbino,ambako wakati mwingine vituo hivyo vilibadilika toka makazi ya muda na kuwa makazi ya kudumu hasa katika mikoa ya mwanza,Simiyu na Kigoma huku akiiomba serikali iichukue jitihada mbali mbali ikiwemo kuwarudisha watoto hao kuendelea kuishi na familia zao huku serikali ikiimarisha ulinzi na kutoa elimu itakayochangia kuondoa imani potofu juu ya albinism.

"Serikali inatakiwa kuendelea kuelimisha umma na kuimarisha hatua za ulinzi kwa sababu jamii kadha wa kadha haziko tayari kuwapokea watoto hawa kutokana na hofu"alisema Bi Ero.

Naye mkurugenzi mkaazi wa shirika la umoja wa mataifa hapa (UN) nchini Antonio Rodriguez amesema umoja wa mataifa utaendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha wanatatua changamoto za kimazingira na kiusalama kwa watu wenye ualbino.

Comments