kampuni ya utunzaji wa mazingira na usafi wa miji ya GreenWaste Pro Ltd inatarajia kukarabati bustani iliyoko eneo la salenda bridge jijini Dar es salaam.

kampuni ya utunzaji wa mazingira na usafi wa miji ya GreenWaste Pro Ltd inatarajia kukarabati bustani iliyoko eneo la salenda bridge(palmBeach)  jijini Dar es salaam.


Akizungumza na wanahabari ofisini kwake meneja mwendeshaji wa kampuni hiyo Abdala Mbena amesema ukarabati wa bustani hiyo iliyopo katika makutano ya barabara ya Ally Hassan Mwinyi na Barack Obama utafanyika wakati wowote kutoka hivi sasa ikiwa ni mkakati wa kampuni hiyo katika kutunza mazingira        "kama mnavyofahamu ndugu waandishi sisi pia ndiyo tuliyoitengeneza na kuikarabati bustani ya sanamu la askari maarufu kama 'askari Monument' iliyopo posta mpya na kuwa katika muonekano mnaouana hivi sasa  kwa kutumia fedha zetu binafsi"alisema Bwana Mbena. 


Muonekano MPYA wa busrani ya sanamu la askari (askariMonument)lililopo posta mpya baada ya kukarabatiwa na kampuni ya GreenWaste Pro Ltd.
Akizungumzia kuhusu kampuni hiyo Mbena amesema kuwa mpaka sasa kampuni hiyo inayojishughulisha pia na uzoaji wa taka imeshatoa ajira  zaidi ya  350 kwa akina mama na vijana sambamba na kushiriki katika kampeni mbali mbali ikiwa ni pamoja na kupanda miti zaidi ya 1600 jijini Dar tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo mwaka 2012 mpaka hivi sasa.          

Kuhusu mafanikio ya kampuni hiyo Mbena amesema kuwa walianza na magari manne tu ya kuzoa taka lakini mpaka hivi sasa wana zaidi ya magari 19 sambamba na kufanikiwa kutoa elimu juu ya utunzaji wa taka Kwani taka ni mali huku akizitaja changamoto za ukosefu wa dampo la kisasa na mazingira magumu ya kuingia na kutoka katika dampo la pugu ambalo liko umbali wa kilomita 30 kutoka mjini jambo ambalo linaleta vikwazo katika shughuli ya uzoaji wa taka kutokana na magari ya taka kutumia muda mwingi katika foleni.

Tuzo mbali mbali ambazo kampuni ya GreenWaste imewahi kushinda kama watunzaji bora wa mazingira.
Kampuni ya GREEN WASTE PRO LTD ambayo ni kampuni ya wazawa ina tenda ya kuzoa taka na kufanya usafi katika wilaya za Ilala,Ubungo na Kinondoni na pia imekuwa ikishinda vikombe mbali mbali ikiwemo mshindi wa kwanza wa utunzaji wa mazingira kimkoa katika mkoa wa Dar es salaam,

Afisa mwendeshaji wa kampuni ya GreenWaste Pro Ltd Abdallah Mbena akizungumza na wanahabari,hawapo pichani
Picha na maktaba.

Comments