RAIS MSTAAFU BENJAMINI WILLIAM MKAPA AFUNGUA JENGO LA UPASUAJI KWENYE KITUO CHA AFYA CHA NKOMO WILAYANI ITILIMA


RAIS MSTAAFU BENJAMINI WILLIAM MKAPA AFUNGUA JENGO LA UPASUAJI KWENYE KITUO CHA AFYA CHA NKOMO WILAYANI ITILIMA

mkap1
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini William Mkapa akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo jipya la upasuaji kwenye kituo cha afya cha Nkomo kilichopo kijiji cha Mwalushu,Wilayani Itilima-Simiyu
mkap2
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Itilima Dkt. Anold Musiba akitoa maelezo kwa Rais Mstaafu,kulia ni Balaozi wa Japan nchini Tanzania Mhe.Masaharu Yoshida. Jengo hilo limejengwa na Ubalozi wa Japan kupitia Taasisi ya Benjamini Mkapa na kugharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 270.
mkap3
Rais Mstaafu akiangalia moja ya vifaa vilivyomo kwenye chumba cha upasuaji .Ujenzi wa jengo hilo kwa asilimia kubwa itawasaidia akina mama wajawazito ambapo awali wananchi wa kijiji hicho walikua wakitembea kilometa arobaini kwenda kupata huduma za namna hiyo.
mkap4
hilo la upasuaji linavyoonekana
mkap5
Msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo kutoka Taasisi ya Benjamini Mkapa Geofrey Nyaluke (mwenye fulana ya jano) akitoa maelezo kwa Viongozi waliofika kushuhudia ufunguzi wa jengo hilo
mkap6
Rais Mstaafu akicheza mara baada ya ufunguzi wa jengo hilo,kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Antony Mtaka na kulia ni Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Daudi Njalu
mkap7
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimulikiwahutubia wananchi wakati wa ufunguzi wa jengo la upasuaji wilaya ya Itilima.
mkap8
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria ufunguzi huo akiwepo mke wa Rais Mstaafu Mama Anna Mkapa
mkap9
Rais Mstaafu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wa awamu ya tatu akihutubia wananchi( hawapo pichani),ambapo aliwataka Watanzania kuongeza hali ya kujiendeleza na kujitegemea ili kutatua changamoto zinazowakabili ili kuweza kufufua pamoja na kukuza uchumi wan chi.
mkap10
Wananchi wa kijiji cha Mwalushu wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa jengo la upasuaji katika kituo cha afya cha Nkomo.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA AFYA)

Comments