Sumaye: Hatuko Tayari Kuzibwa Midomo na Serikali

Sumaye: Hatuko Tayari Kuzibwa Midomo na Serikali

Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Halmashauri  Kuu Chadema, Frederick Sumaye amesema kuwa licha ya kukatazwa wasizungumze masuala ya kisiasa, lakini hawatanyamaza.

Akizungumza na vyombo vya habari leo, Sumaye amesema kuwa wataendelea kufanya kazi kwa niaba ya wananchi ambao wana imani nao.

Amesema nchi  kwa sasa inakazana kujenga mfumo wa demokrasia kandamizi ambayo kwa kiasi kikubwa inarudisha nyuma maendeleo.

"Viongozi wa upinzani wamekuwa wakikamatwa, wanawekwa rumande, wanatishwa lengo ni kudhoofisha upinzani," amesema Sumaye.

Amesema licha ya juhudi hizo za kuwarubuni baadhi ya viongozi wakiwamo madiwani wachache, hawatadhoofika na wataendelea kufanya Kazi.

Sumaye amesema kwamba  wanataka kujenga upinzani  wa kweli wenye lengo la kusaidia wananchi.

Amesema katika kulihakikisha hilo hadi kufikia mwaka 2018 hakutakuwa na kijiji, mtaa utakaokuwa hauna tawi la Chadema

Comments