CHANGAMOTO ZA MAJI KUPATIWA UFUMBUZI DAR ES SALAAM.

Kaimu mkurugenzi WATERAID,HENRY HOROMBE.

Imeelezwa kuwa licha ya maji mengi yanayozalishwa na kufikia kukidhi zaidi ya  asilimia 90 ya wananchi jijini Dar es salaam lakini bado maji hayo hayajawafikia wananchi wengi kutokana na uhaba wa mtandao wa miundombinu yake.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam katika mkutano wa wadau wa maji,mkuu wa wilaya ya Ilala Bi Sophia Mjema amesema kuwa hali hiyo imechangiwa na uhaba wa mabomba hususan ni maeneo yaliyoendelezwa miaka ya hivi karibuni na yale yaliyoko pembezoni mwa jiji.

Bi  Mjema amesema kuwa mkoa wa Dar es salaam utahakikisha unatatua changamoto hizo ikiwa ni pamoja na kero na malalamiko mengi yanayotoka kwa wananchi  kupitia mamlaka za Dawasa na Dawasco ili wananchi wake wawe wanapata maji safi na salama kwa asilimia 95 kufikia mwaka 2020 huku akiipongeza benki ya dunia na serikali ya Korea ya kusini kwa kukubaki kufadhili miradi mkubwa ya maji na Usafi wa mazingira jijini Dar es salaam.


Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa taasisi ya WATERAID Bw HENRY   HAROMBE amesema kuwa zaidi ya bilioni 17 zinahitajika ili kukidhi na kutatua  changamoto mbali mbali za maji ambazo zinalikabili jiji la Dar es salaam huku akiwaomba wadau mbali kujitokeza na kuunga mkono taasisi hiyo kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za maji.

Naye  Kaimu mkurugenzi wa  usambazaji na uzalishaji wa maji (DAWASCO)Mhandisi HARON JOSEPH amesema Dawasco itahakikisha wananchi wa mkoa wa Dar es salaam wanapata huduma bora za maji kwa kuhakikisha wanaiboresha miundombinu ya maji na kufikia mkakati wa kushirikiana na wadau mbali mbali wa maji ili kufikia lengo la mkoa huo wa zaidi ya asilimia 95 ya wananchi kupata maji safi na salama kufikia mwaka 2020

Comments