MAENDELEO YA UBORESHWAJI WA UTOAJI HUDUMA HOSPITAL MPYA YA WAZAZI CHANIKA YAMFURAHISHA MKUU WA MKOA WA DSM

MAENDELEO YA UBORESHWAJI WA UTOAJI HUDUMA HOSPITAL MPYA YA WAZAZI CHANIKA YAMFURAHISHA MKUU WA MKOA WA DSM

Rc Makonda akiwa hutubia baadhi ya watumishi watakao hudumu katika hospital ya chanika ya Mama na mtoto ambayo inatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania 

Mganga mkuu wa mkoa Dar es salaam Dk Grace Maghembe Akitoa maelekezo na ufafanuzi kwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuhusu watumishi mbali mbali watakao toa huduma katika hospital ya Chanika Ya Mama na Mtoto pamoja na huduma mbali mbali zitakazo endeshwa katika hospital hiyo.
Rc Makonda akipokea maelekezo toka kwa mganga mkuu wa wilaya ya ilala Dk Victorina Ludovick kuhusu namna alivyojipanga katika kuhakikisha hospitali hiyo inatoa huduma bora na yenye kuwa mfano wa kuigwa katika wilaya,mkoa hadi ngazi ya Taifa.
Meya wa manispaa ya wilaya ya Ilala Charles Kuyeko akizungumza na watumishi watakao hudumu katika hospital hiyo ya mama na mtoto mara tuu baada ya kuanza kwa huduma katika hospitali hiyo mbele ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam aliefika kwa ajili ya kuwatambua atumishi mbali mbali watakao toa huduma kwenye hospitali hiyo pamoja na kutazama maendeleo ya hospitali hiyo.

Hawa ni baadhi ya watumishi ambao watatoa huduma katika hospital ya mama na mtoto chanika walipo kuwa wakimsikiliza Rc Makonda alipoitembelea  Hospital hiyo siku ya Leo.
  Rc Makonda akisikiza maelekezo toka kwa mmoja wa kutoa huduma katika idara ya  mapokezi katika hospital ya mama na mtoto chanika alipoitembelea hospitali hiyo inayotarajiwa kuanza kutoa huduma baada ya siku sio nyingi kuanzia sasa 


Muonekano wa ndani wa chumba cha hospitali hiyo ambayo tayari vifaa vyote vimekwisha kamilika.


Dar es salaam


MKuu wa mkoa wa Dar es salaam  mhe. Paul  Makonda  amewataka watumishi wa Afya wa Manispaa ya ilala kufanya kazi kwa bidii na kuwajali na kuwasikiliza wagonjwa kwa lugha nzuri kwa  kuwa kazi hiyo nikazi ya wito na wawahudumie wananchi bila kuja itikadi zao za kisiasa .

Mhe. Makonda ameyasemahayo leo  wakati anazungumza na watumishi wa Hospital ya Mama na Mtoto iliyoko Chanika katika Manispaa ya Ilala iliyojengwa  kwa Ufadhili wa serikali ya Korea kusini , ambayo tayari imetengewa watumishi na inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni nakuwataka kutoweka mbele Zaidi maslahi yao binafsi.

“Fanyeni kazi Msipolipwa Duniani  Mungu atawalipa mbinguni, motive ya m fanya kazi bora siyo mshahara bali ni huduma nzuri anayeweka mbele pesa huyosiyo mfanyakazi bora, serikali inafanya juu chini kuwa ongezea watumishi mishahara, na tutaendelea kuboresha mzingira yakazi na kwasasa tutawakopesha viwanja mtalipa kidogokidogo ndani ya miaka minne na tayekuwa na uwezo atalipa kwa muda wa mwaka mmoja.”Alisema Makonda

“Ninyi kazi yenu nikama mchungaji ama shekhe ,Unapoammka asubuhi ombi lako kwa wa gonjwa liwe kuwaombea uzima wagonjwa nawala siyo  kuwaombea mauti ”Aliongeza  Makonda

Hospital ya mama na mtoto chanika niyakisasa na imewekwa vifaavyote vipya ambapo inatarajiwa kuwa itapunguza msongamano katika hospital ya amana ilala na kuleta unafuu kwa wanachi wa cahanika na maeneo jira katika kufuata mbali huduma za afya.

Kwa upande wake mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Grace Mghembe amewashukuru KOICA  na kuahidi kuwa  kwa upande wahuduma watatoa huduma nzuri  na watapanga watumishi katika hospital hiyo pamoja na upungufu wa watumishi uliopo anasema wameomba kibali utumishi na wakisha patiwa  watumishi watapangwa katika hospitali hiyo.

Naye Meya wa Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko amempongeza mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mhe Paul Makonda  kwa uchapakazi na kujitoa kwake katika kuboresha huduma za afya mkoani humo na kutatua kero za wananchi “Ndugu zangu hakuna atakayepinga hili nikweli Makonda anafanya vizuri nikatika wakuu wa mikoa wachache sana wanachapakazi.

Kwa upande wake  mganga mkuu wa  wa manispaa ya Ilala  Victorina Ludovick amesema  vifaa ambavyo vilikuwa havija timia vyenye thamani ya  shilingi  million  100, vikonjiani kutoka Corea vina kuja na vingine kutoa MSD navyo vita wasili wiki ijayo  na changamoto ambayo bado ipo ni uzio ambao bado ni wa mabati na wamepangiwa wtumishi 78 wakuanza ana baadaye wengine watapangiwa .

“ Halmashauri  imetenga shilingi million 600 mwaka huu kwaajili ya matumizi ya hospital hii  ni kidogo kwakuwa mahitaji halisi ni shilingi Bilion 1.5 .” Alisema  Ludovick

Comments