WAKAZI WA DAR ES SALAAM SASA KUPATA MAJI YA KUTOSHA.

WAKAZI WA DAR ES SALAAM SASA KUPATA MAJI YA KUTOSHA.

ASAZ
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitazama mambo ya kupitishia maji ikiwa ni pia sehemu ya miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar
AWZ
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipewa maelezo mafupi juu ya muundo mzma mzima wa miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar
GTHTH
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitazama miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar
WSWD
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akishiriki kuchimba mtaro wa kupitisha bomba la maji ikiwa ni sehemu ya miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar.
……………………………………………………………………
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda jana amefanya ziara ya ukaguzi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa Maji ya kutosha kwa Wakazi wa Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo Makonda ametembelea Ujenzi wa Vituo vya Usambazaji wa Maji, Visima pamoja na maeneo yatakayojengwa mifumo ya kisasa ya kusafirisha na kutibu Maji taka.
Makonda amesema lengo la Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli ni kumtua Mama Ndoo kichwani na kuhakikisha huduma ya Maji inawafikia Wananchi wote.
Amesema kukamilika kwa miradi ya Ujenzi wa Vituo Vinne vikubwa vya usambazaji wa Maji vinavyojengwa maeneo ya Changanyikeni, Makongo, Wazo na Bunju*vitasaidia kuzalisha Maji ya kutosha na kutatua kero kwa Wananchi.
Katika ziara hiyo pia Makonda ametembelea Visima 10 ambavyo aliahidi kwenye Ziara ya Dar Mpya ambavyo Ujenzi wake umekamilika vikiwa na uwezo wa kuzalisha Lita 16,000 kwa kila kisima ambavyo vitahudumia wakazi wa Wilaya ya Ubungo.
Aidha Makonda ametembelea eneo la Jangwani ambapo  kutajengwa Mfumo wa Maji taka utakaogharimu kiasi cha Bilion 200 na eneo la Kilongawima Mbezi Beach kunakojengwa mfumo wa Maji taka utakaogharimu kiasi cha Bilion 135 chini ya ufadhili wa Bank ya Dunia na Serikali ya Japan.
Hata hivyo amesema bado Serikali inaendelea kufanya jitiada za kuhakikisha Wakazi wa Wilaya ya Kigamboni na Temeke wanapata maji ya kutosha kupitia miradi mbalimbali inayoendelea.
Amewataka Wananchi ambao bado hawajaunganishwa na huduma ya Maji kufika Ofisi za DAWASCO ili waunganishiwe Maji bila malipo ambapo baada ya hapo watawekewa utaratibu wa malipo.

Comments