WAZIRI TIZEBA AWATAKA WATENGENEZAJI NA WASAMBAZAJI W MBOLEA KUTOA ELIMU KWA WAKULIMA.
Waziri wa KILIMO,Mifugo na Umwagiliaji Dr.Charles Tizeba amewataka wadau wa mbolea kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa wakulima kwa kutoka elimu ya namana ya matumizi bora ya mbolea kulingana na sina ya udongo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano w pili uliyowakutanisha wadau wa mbolea Dr.Tizeba amesema kuwa kuna wakulima hadi sasa hawajawahi kuona wala kushika mbolea wakati wa sgughuli zao za KILIMO hivyo wadau wa mbolea hususani makampuni yanayosambaza na watafiti mbalimbali wa masuala ya kilimo washirikiane na serikali katika kuwasidia wakulima kwa matumizi ya mbolea.
Aidha amesema kuwa serikali imefuta tozo mbalimbali katika ekta ndogo ya mbolea ili kusaidia wakulima na wafanyabiashara wa mbolea kunufaika kwa pamoja ili kuleta maendeleo katika maisha ya wakulima.
Amesema kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua stahiki kwa wafanyabiashara ambao watakiuka maekekezo ya bei ya serikali kwa kuuza mbolea kwa gharama kubwa huku serikali imeondoa baadhi ya kodi.
"Asilimia 65 ya watanzania ni wakulima,tunataka tuone maisha ya wakulima huko vijijini yanabadilika,hivyo shughuli yenu hapa nikuwaza namna yakumbadilisha mkulima wa Tanzania
"Alisisitiza Dr.Tizeba.
Kwa upande wake Mkuu wa shirika la maendeleo ya kijani katika kilimo barani Afrika(AGRA) Bw .Nuhu Hatibu amemkabidhi Dr.Charles Tizeba kitabu cha utafiti wa masuala yanayomkwamisha mkulima kutumia mbolea na namna ya kukabiliana na changamoto hizo,ambapo utafiti huo umefanywa na shirika hilo katika nchi zaidi ya11 barani afrika ikiwemo Tanzania.
Akizungumza mmoja wa wadau wa sekta ya mbolea Afisa masoko kutoka kiwanda cha mbolea cha minjingu Project Amosi amesema kuwa wamefurahishwa na nia ya serikali yakuhakikisha inaweka mikakati mizuri ya kuboresha sekta ya kilimo kwa kuhakikisha mbolea inazalishwa kwa wing na kuuzwa kwa bei nafuu.
Mkutano huo una malengo makubwa ya kujadili namna ya kuongeza matumizi ya mbolea,upatikanaji wa mbolea,bei nafuu ya mbolea atakayoweza kuimudu mkulima pamoja na teknolojia za kisasa katika kuendeleza sekta ya kilimo.
MWISHO
"Alisisitiza Dr.Tizeba.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tzeba akiongea na wadau wa Mbolea wa Tanzania alipofungua mkutano wao katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam. |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Eng. Mathew Mtigumwe akitambulishwa kwa wadau. |
Wadau wa Mbolea wa Tanzania wakifuatilia mada katika mkutano wao Dar es Salaam. |

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tzeba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam. |
Comments