KITUO KIKUBWA CHA USAMBAZAJI WA BIDHAA ZA UJENZI KUJENGWA NCHINI

KITUO KIKUBWA CHA USAMBAZAJI WA BIDHAA ZA UJENZI KUJENGWA NCHINI

Waziri Wa Viwanda Na Uwekezaji Mhe Cherles Mwijage, Balozi Wa Serikali Ya Jamhuri  Ya Watu Wa China Nchini Tanzania Bi Wang Ke Wakizindua Ujenzi Wa Kituo Cha Usambazaji CNBM Tanzania Ltd mapema leo jijini Da es salaam, 







Waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji Charles Mwijage 


  • DAR ES SALAAM.
Waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji Charles Mwijage ameweka jiwe la msingi kuashiria kuaza kujengwa kwa kituo kikubwa cha usambazaji wa bidhaa za ujenzi hapa nchini.

Ujenzi wa kituo hicho kikubwa kinakadiriwa kugharimu Jumla ya  dola milioni 75 za kimarekani  ambazo zinatarajiwa kujenga  majengo matatu ya usambazaji bidhaa za ndani nchini,  chini ya kampuni ya uuzaji wa vifaa vya ujenzi kutoka China (NBMG).


Akizungumza katika uwekaji wa jiwe la  msingi eneo la Tabata-Matumbi jijini Dar es Salaam ,Waziri  Charles Mwijange, amesema kuwa kituo  hicho kitakuwa kikisambaza vifaa vya ujenzi na  kitawasaidia Watanzania kujipatia ajira na kuongeza ufanisi kwa vijana nchini kwa kunufaika na kituo hicho huku akiwaomba wawekezaji hao kuangalia jinsi wanavyoweza kuongeza uzalishaji wa mihogo, pamba na utengenezaji wa nguo kwa sababu maeneo yote hayo bado yanatafuta wawekezaji.

Kuhusu suala la usumbufu kwa wawekezaji waziri mwijage amesema kuwa  atawaondoa watu wote wanaokwamisha wawekezaji na utoaji wa mizigo bandarini kabla hajatolewa yeye na hivi sasa ameanza kazi ya kuchuka majina ya watu wote walio chini yake ili kuanza kuwafatilia.

 Aidha amesema Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na serikali ya Tanzania itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wenye nia njema kwa serikali hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda.


Aliwapongeza pia watu wote wenye nia ya kuwekeza hapa nchini katika miradi mbalimbali ya viwanda kwa upande wa mazao kama vile muhogo, zao ambalo sasa ni muhimu na lenye kuweza hata kuuzika nje ya nchi.

Naye Balozi mpya  wa China hapa nchini, Bi Wang Ke, amempongeza Mwenyekiti wa kampuni hiyo ya CNBM, Song Zhiping, kwa kuanzisha kituo hicho ambacho kitakuwa muhimu na kitatoa fursa fursa kwa wakazi wa maeneo hayo katika kupata ajira. 

 

 
Balozi mpya  wa China hapa nchini, Bi Wang Ke, akizungumza katika uzinduzi huo.


Mwonekano Wa Jengo La Kituo Cha Usambazaji CNBM Tanzania Ltd Mara Baada Ya Kukamilika Ujenzi Wake.


 Mwenyekiti Wa Bodi ya CNBM Group Co Ltd Dkt. Zhiping Song Akizunguza Wakati wa uzinduzi wa Ujenzi wa Jengo la Kituo cha Usambazaji CNBM Mapema leo Jijini Dar es Salaa.

Comments