WABUNGE 8 WALIOVULIWA UANACHAMA CUF WATAKA KUREJESHEWA UBUNGE WAO MARA BAADA YA MAHAKAMA KUWATAMBUA KAMA WANACHAMA.

WABUNGE 8 WALIOVULIWA UANACHAMA CUF WATAKA KUREJESHEWA UBUNGE WAO MARA BAADA YA MAHAKAMA KUWATAMBUA KAMA WANACHAMA.




Wabunge nane wa viti maalum ambao waliovuliwa uanachama wa chama hicho na ile inayojiita kamati ya maadili ya CUF inayoongozwa na Upande wa Profesa Ibrahim LIpumba wameiandikia barua ofisi ya bunge kutaka kurejeshewa nafasi zao za ubunge ambazo bunge liliwavua na kuwaapissha wabunge wengine nane

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Dar es salaam hii leo kwa niaba ya wabunge hao  kiongozi wa wabunge hao waliovuliwa ubunge miezi kadhaa iliyopita Bi SHAHARI MNGWALI amesema mara baada ya mahakama kuu ya tanzania kanda ya Dar es salaam kuitaka cuf isijadili uanachama wa viongozi hao na kutengua uamuzi wa cuf wa kuwavua wabunge hao uanachama wamemwandikia barua katibu wa bunge november 20,2017 wakimtaka kulitaarifu bunge na spika wa bunge kuwarejesha tena bungeni kama wabunge halali wa CUF .




Comments