Watoto 20 wenye matatizo ya moyo wafanyiwa upasuaji bila kufungua kifua [JKCI]Muhimbili.
DAR ES SALAAM
Watoto 20 wenye matatizo ya moyo wafanyiwa upasuaji bila
kufungua kifua [JKCI]Muhimbili.
Taasisi ya moyo ya Jakaya kikwete kwa kushirikiana na
taasisi ya okoa moyo wa mtoto{save a child heart-SACH] ya nchini Israel kwa
watoto 20 wenye matatizo ya moyo.
Mkurugenzi wa tiba wa taasisi hiyo dkt Peter Kisenge amesema
leo jijini Dar es salaam kuwa upasuaji huo unatumia mtambo wa cathlab
umefanyika katika kambi maalum ya matibabu ambayo inamalizika kesho kwa kuziba
matundu kwenye moyo na kutanua mishipa ya moyo.
‘’katika kambi hii tunatarajia kufanya uchunguzi kwa watoto
100 kati ya hao watoto 60 ambao watakuwa na matatizo makubwa watapelekwa nchini
Israel kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua mwakani na watoto 40
watatibiwa hapa nchini’’amesema dkt kisenge.
Aidha kwa upande wake mkurugenzi wa taasisi ya save a childs
heart,Simon Fisher amesema taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na taasisis ya
moyo ya jakaya kikwete kwa miaka kadhaa sasa na kuwawezesha madaktari mbali
mbali kwenda nchini Israel kujifunza namna ya kufanya upasuaji wa moyo huku
akiishukuru taasisi hiyo kukubali kushirikiana nao kuokoa watoto wenye matatizo
ya moyo hapa nchini.
Hata hivyo taasisi ya moyo ya jakaya kikwete itakuwa na
kambi nyingine hapo kesho kwa watoto na watu wazima ambayo itafikia tamati November
27 mwaka huu kwa kushirikiana na taasisis ya open heart international ya nchini
Australia.
Comments