AGA KHAN YAZINDUA KITUO KIPYA CHA AFYA KIGAMBONI
AGA KHAN YAZINDUA KITUO KIPYA CHA AFYA KIGAMBONI
Katibu tawala wa Wilaya ya kigamboni Rachael Muhando akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo hicho cha afya akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wa hospitali ya aga khan |
Taasisi ya huduma za afya Aga Khan tawi la kigamboni jijini Dar es Salaam imetakiwa kutoa huduma ya matibabu kwa bei nafuu kwa lengo la kuwafikia wananchi wa kipato cha chini.
Hayo yamesemwa leo na Katibu tawala wa Wilaya ya kigamboni Rachael Muhando wakati wa uzinduzi wa Hospitai ya Aga Khan tawi la kigamboni na kutoa rai kwa taasisi hiyo kutoa huduma za matibabu kwa bei nafuu ili waweze kuwapa fursa wakazi wa maeneo hayo kupata huduma za afya kutoka katika hosptali hiyo.
" Kufunguliwa kwa kituo hiki ni fursa nzuri kwa wananchi wote hasa wakazi wa kigamboni kupata huduma iliyo bora"Amesema Muhando.
Amesema kuwa ni faraja na furaha kuona upanuaji wa huduma za afya kwa kuongeza hospitali karibu zaidi zinazotolewa na kusaidia kupunguza, kuondoa kwa kiasi kikubwa wagonjwa wanaokwenda kutafuta huduma nje ya nchi.
Aidha ametoa with kwa watoa huduma wote wa Taasisi hiyo kutumia lugha ya kitabibu wakati wanapohudumia wagonjwa wao kwani kwa kufanya hivyo kunachangia kuongeza faraja na afueni kwa wagonjwa wanofika hopitalini hapo.
Bi Muhando amewataka watanzania kuchukua taadhari ya Ugonjwa wa UKIMWI kwani kinga ni bora kuliko tiba na kuwataka wananchi kutowatenga na kutokuwanyanyapaa wenye Ugonjwa huo ukuzingatia leo ni Siku ya Maadhimisho ya Ugonjwa huo duniani note.
"Leo ikiwa ni siku ya UKIMWI duniani Kila mwananchi anapaswa kuchukua tahadhari has a ukizingatia Ugonjwa huu hauna tuba hivyo kinga ni bora zaidi" amesema Bi.Muhando
Kwa upande wake Mkurugenzi Uendeshaji wa vituo Afya Aga Khan Tanzania Bw. Fayyaz Mohamed amesema huduma zitatolewa ni zile zile zinazotolewa katika hospital ya Aga khan ni zile zile na kuwataka wananchi kuacha kufikiri kuwa hopitali hiyo ni ya matajiri tu, amewatoa hofu kwani mtu yeyote mwenye kipato cha chini na cha huu wanaweza kutibiwa hapo.
Ameongeza kuwa watahakikisha tawi hilo la hospitali ya Aga Khan kigamboni wanajiunga na Bima ya Afya NHIF ili kurahisisha matibabu kwa wananchi na wakazi wa maeneo ya karibu.
Naye Mkurugenzi wa Uuguzi Taasisi za huduma za Afya Aga Khan Tanzania Mama Lucy Hwai amesema wamefungua kitengo maeneo ya kigamboni ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma kwa urahisi zaidi, na kusema huduma zitakazotolewa ni za Mama na mtoto pamoja na matibabu mbalimbali.
"Niwaombe wananchi na wakazi wa maeneo haya kuweza kutumia huduma hii kwani imerahisishwa kwa kuletwa karibu kabisa ili kila mtu aweze kupata kwa urahisi kabisa" Amesema Lucy Hwai.
Comments