Kampuni kubwa ya kazi za sanaa Afrika mashariki [BARAZANI] yazinduliwa Tanzania
Kampuni kubwa ya kazi za sanaa Afrika mashariki [BARAZANI] yazinduliwa Tanzania
| Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akikata utepe leo Jijini Dar es Salaam kuashiria ufunguzi wa Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji wa kazi za Filamu hapa nchini. |
| Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Tyeeo Entartainment Bw.John Kalaghe wakati wa ufunguzi wa Mradi wa Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji wa kazi za Filamu hapa nchini uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fissoo |
| Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akikata utepe leo Jijini Dar es Salaam kuashiria ufunguzi wa Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment inayohusika na usambazaji wa kazi za Filamu hapa nchini. Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati) na viongozi wa Kampuni ya Tyeeo Barazani Entertainment wakionyesha Filamu ya “Queen of Masai”itakayoanza kusambazwa na Kampuni hiyo kuanzia kesho. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisso
Kampuni mpya nchini Tanzania ijulikanayo kama Barazani Intertainment jana iliziinduliwa rasmi ili kuanza kazi zake za usambazaji wa kazi mbali mbali za sanaa ikiwemo filamu za ndani yaani bongo movie na hata zile filamu zilizotiwa maneno ya kiswahili
Ujio wa kampuni hiyo mpya hapa Tanzania unaweza ukawa ni mwarobaini wa wizi wa kazi za wasanii hapa nchini kutokana na kazi zao kuibiwa na hatimaye kuwafanya wasanii kukosa kipato stahiki kutokana na kazi zao za sanaa.
Tyeeo Barazani Entertainment itakayohusika na usambazaji wa kazi za Sanaa kuanzia kesho.[LEO]
Serikali kupitia waziri wa sanaa Dkt Harryson MWAKYEMBE imesema kuwa itaendelea kuwachukulia hatua wote watakaobainika kusambaza kazi za sanaa kinyume na utaratibu ili kuondoa kero ya muda mrefu ya wizi wa kazi za Sanaa uliolalamikiwa na wasanii wote hapa nchini.
“Serikali haitaendelea kuwafumbia macho wezi wa kazi za Sanaa,tutawashughulikia kama ambavyo tumeanza na mafanikio yameanza kuonekana yeyote anaetaka kusambaza kazi hizi aende Barazani Entartainment watamsaidia.”Alisema Dkt Mwakyembe.
Aidha amewataka wasanii wote hapa nchini kutumia Kampuni hiyo kwa manufaa ili waweze kupiga hatua ambapo pia amewahakikishia kuwa ndani ya kipindi kifupi kijacho sekta ya Sanaa itakuwa na mageuzi makubwa.
Katibu wa Bodi ya Filamu nchini Bibi. Joyce Fissoo amewahakikishia wasanii hao kuwa Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Wilaya wapo tayari kushirikiana na Kampuni ya Barazani Entartainment katika kuleta mafanikio ya kazi zao.
kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw.John Kalaghe ameishukuru Serikali kwa ushirikiano ilioupatia kampuni hiyo tangu ilipoanzisha wazo hilo ambalo leo limefanikiwa na wasanii wataanza kunufaika na kazi zao kwani Kapuni hiyo itasambaza kazi zao kwa urahisi na salama zaidi.
Kampuni ya Tyeeo Barazani Entartainment itakuwa ndio wakala wa kusambaza kazi za sanaa ikiwemo Filamu za nje na ndani,Muziki,masomo ya watoto,na makala za kielimu kupitia simu ya mkononi kwa mitandao yote kwa malipo nafuu.
|


Comments