Mtanzania liyeshinda taji la dunia la urembo awasili nchini,apokelewa kwa shangwe
Mtanzania aliyeshinda taji la dunia la urembo awasili nchini,apokelewa kwa shangwe
Tanzania imeingia Katika headines tena duniani mara baada ya mtanzania kuchukua taji la dunia Katika mashindano ya miss world university yaliyofanyika nchini Cambodia.
Mrembo huyo wa kitanzania QUEEN ELIZABETH MAKUNE ambaye ni
mtanznia wa kwanza kuchukua taji hilo amerejea leo nchini Katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius nyerere international airport ambapo alilakiwa na
mamia ya watanzania wakiwemo ndugu,jamaa na marafiki ambao walionyesha furaha zao pindi mrembo huyo
lipoingia nchini.
Awali akizungumza mara baada ya kuwasili na ndege ya shirika
la ndege la Emirates QUEEN ELIZABETH amewaambia wanahabari kuwa kujiamini kwake
ndiko kulimfanya kushinda taji hilo la WORLD MISS UNIVERSITY AFRICA [Continenta
queen of Africa] Katika masuala ya amani ambalo warembo kutoka nchi mbali mbali
duniani walikuwa wakilishindania.
Mlimbwende huyo ameongeza kuwa atakuwa balozi mzuri wa amani
Katika bara la afrika na kuiwakilisha vyema bendera ya Tanzania Katika nchi za
afrika.
Naye katibu mtendaji wa baraza la sanaa la Taifa ngereBw Charles Ngereza akizungumza kwa niaba ya waziri wa habari,utamaduni,sanaaa na michezo amesema
serikali imefurahishwa na ushindi wa mlimbwende huyo ambaye ameiletea sifa
kubwa nchi ya Tanzania na itahakikisha inashirikiana naye hasa Katika sauala
amani
kwa upande wake mratibu wa mashindano hayo kwa hapa nchini
aiyejitambulisha kwa jina la Frank amewaambia wana habari kuwa kampuni yake
itaendelea kushiriki Katika mashindano hayo na itahakikisha mataji mengi kama
hayo yanakuja hapa nchini.
Hata hivyo kwa upande wake mama mzazi wa mrembo huyo wa
dunia na afrika ESTER JOHN KILOBA amesema amepata furaha mara baada ya binti
yake kushiriki mashindano hayo na kushinda huku akiwataka wazazi ambao wanaona
mashindano ya urembo kuwa ni uhuni kuachana na dhana hiyo.
QUEEN ELIZABETH MAKUNE ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha
Tanzania Institute of Accoutance [TIA]
amekuwa ni mtanzania wa kwanza kushinda taji hilo Katika bara la afrika na
kuifanya Tanzania kujitangaza vyema kimataifa Katika tasnia ya ulimbwende
yaliyohusisha nchi mbali mbali duniani ukiachana na Nancy Sumary aliyeshinda taji
linalofanana na hilo miaka kumi iliyopita
Comments