MWANAMUZIKI VANESSA MDEE AZINDUA RASMI ALBAM YAKE YA KWANZA YA MUZIKI,MAHOMBI ADONDOKA BONGO KUMPA SHAVU.

MWANAMUZIKI VANESSA MDEE AZINDUA RASMI ALBAM YAKE YA KWANZA YA MUZIKI,MoHOMBI ADONDOKA BONGO KUMPA SHAVU.












Suala la albam kwa wasanii wengi wa kibongo limekuwa ni kama pasua kichwa kutokana na wasanii wengi kuamini zaidi Katika kutoa hit songs tu huku wengi wakiogopa kutoa albam.
Lakini kwa mwanamuziki VANESSA MDEE jambo hil halikuwa gumu kwake mara baada yam kali huyo anayetamba na wimbo wa BOUNCE kuachia albam yake inayokwenda kwa jina la MONEY MONDAYS ikiwa ni siku chache tangu mwanamuziki huyo kusainiwa ya lebo ya muziki ya kimataifa ya UNIVERSAL

Albam ya mwanamuziki Vanessa mdee imezinduliwa na mkali aliyeshinda tuzo ya kimataifa ya grammy mwenye uraia wa Sweden na congo MOHOMBI ambaye alikuja nchini  nchini kwa ajili ya shughuli hiyo
.
Hata hivyo Katika uzinduzi wa albam hiyo uliyofanyika Katika hoteli ya hyatt regency,Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam ambapo walialikwa watu maalum wakiwemo mastar mbali mbali sambamba na mwanadada huyo kuzindua wimbo wake mpya ‘’KWANGU NJOO’’ aliyomshirikisha mkali wa kimataifa MOHOMBI.



Katika albam hiyo wameshirikishwa wakali mbali mbali akiwemo joh makini,Caspper Nyovest wa afrika kusini na wakali wengine
Uzinduzi wa albam hiyo umeratibiwa na kusimamiwa na mkito app pamoja na wadhamini wengine wakiwemo GSM travel and tours,Hyatt regency na hennesy







Comments