SBC Tanzania Limited kumwaga mamilioni kwa wateja, wake yazindua shindano la jishindie mamilioni.

SBC Tanzania Limited kumwaga mamilioni kwa wateja, wake yazindua shindano la jishindie mamilioni.



Pepsi 1
Meneja Mafunzo na Uwezeshaji toka Kampuni ya SBC  Rashid Chenja (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa shindano la Jishindie Mamilioni mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Afisa Habari toka Idara ya Habari (MAELEZO) Frank Shija na kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Roselyne Bruno.


Kampuni ya SBC Tanzania Limited imeanzisha shindano kabambe litakalojulikana kwa jina la “Jishinde Mamilion”linalohusu soda aina ya Pepsi,Mirinda Orange,Mirinda Fruity,Mirinda Green Apple,Mountain Dew(300ml)  pamoja na Seven up za ujazo wa mililita 350.

Meneja Mfunzo na Uwezeshaji wa Kampuni ya SBC Tanzania Limited Rashid Chenja amezungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema lengo la shindano hilo ni kuongeza unywaji wa soda na kuipatia jamii sehemu ya faida ili kuwawezesha kujikomboa kiuchumi.

“Shindano hili litaanzishwa kuanzia tar.4/12/017 mpaka 14/1/2018 katika baadhi ya mikoa nchini ikiwemo Dar es salaam,Pwani,Morogoro,Dodoma,Tanga,Lindi pamoja na Mtwara”amesema Cheja

Hata hivyo Bw.Chenja amesema vizibo vya shindano hili vitakuwa na rangi ya silva ambapo kutakuwepo na zawadi za pesa taslimu kiasi cha shilingi 1,000,000/,500,000/-,10,00/-,5000/-,1000/- na soda ya bure.

“Ili mteja ajishindie zawadi anapaswa kununua soda za jamii ya Pepsi kasha abandue ganda ndani ya kizibo akikuta maandishi aidha ya shilingi 1,000,000/-,500,000/-10,000/-1000/-shilingi 5000/-1000/-,na soda ya bure zitapatikana kwa aliyeuza soda,gari ya mauzo au Muuzaji wa Jumla”alisema Bw. Chenja

Kampuni ya SBC Tanzania Limited  ni watengenezaji na wasambazaji wa vinywaji  aina ya Pepsi,Mirinda,7up na Mountain Dew 


Pepsi 2
Meneja Masoko wa Kampuni ya SBC  Roselyne Bruno (kushoto) akionesha ya kizibo chenye zawadi ya soda ya bure kwa waandishi wa habari (hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa shindano la Jishindie Mamilioni mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Afisa Habari toka Idara ya Habari na katikati ni Meneja Mafunzo na Uwezeshaji wa Kamuni hiyo  Rashid Chenja.



Comments