TRL YAFUFUA KICHWA CHA TRNI CHA MWAKA 1954 KINACHOTUMIA MVKE KUJIENDESHA,WAKAZI WA DAR KULA NACHO BATA KUANZIA KESHO

TRL YAFUFUA KICHWA CHA TRENI CHA MWAKA 1954 KINACHOTUMIA MVUKE KUJIENDESHA,WAKAZI WA DAR KULA NACHO BATA KUANZIA KESHO




Kampuni ya reli tanzania TRL imekifufua kichwa {injini} cha garimoshi kilichoanza kutumika nchini kabla ya uhuru mwaka 1954 ambacho ndicho kichwa pekee kizima kilichobaki katika nchi za afrika mashariki na kati.

Akizungumza na wanahabari hii leo katika eneo la pugu nje kidogo ya jiji la Dar es salaam katika majaribio ya kichwa hicho{injini]Mkurugenzi mtendaji wa TRL,Masanja kadogosa amesema wameamua kukifufua kichwa hicho ili kurejesha kumbukumbu za kale kwa watanzania sambamba na kuwapa fursa wananchi kukiona na kukitumia

"injini hiyo iliyopewa jina la SUK yaani SUKUMA tangu enzi hizo na nyinginezo nyingi zililzokuwa na majina ya makabila kama vile CHAGGA n.k zilifanya kai miaka 30 kuanzia 1954 hadi 1984 ambapo teknolojia hiyo haikuweza tena kuendelea kutokana na kuanza kuingia kwa teknolojia mpya ya injini za dizeli"alisema Bw KADOGOSA

Aidha ameongeza kuwa kuanzia kesho hadi jumatatu wakazi wa dar es salaam watapata fursa ya kupanda treni hiyo itakayofanya safari kutoka dar hadi pugu sambamba na kusheherekea sikukuu ya krismasi katika eneo la pugu ambapo kutakuwa na huduma mbali mbali za vyakula na vinywaji pamoja na wasanii 

Comments