Tutapambana kuhakikisha tatizo la sumu kuvu linamalizika nchini ,TFDA
Tutapambana kuhakikisha tatizo la sumu kuvu linamalizika nchini ,TFDA
![]() |
| mkurugenzi mkuu wa TFDA, Hiiti Silo |
Sumu kuvu ni aina ya kemikali za sumu inayozalisha ukungu au fangasi kwenye mbegu za nafaka kama mahindi, kunde na karanga.
Kutokana na tatizo hilo kuwa kubwa mamalaka mbali mbali zinaendelea kulitafutia ufumbuzi.
mkurugenzi mkuu wa TFDA, Hiiti Silo amewaambia wanahabari kuwa mamlaka ya chakula na dawa nchini itahakikisha suala hilo linapatiwa mwarobaini ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufunga mkutano wa siku mbili uliwakutanisha wataalam kutoka nchi 15 za Afrika.
Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kujadili mikakati ya kudhibiti sumu kuvu katika nafaka.
“Kwa sababu kama ambavyo taarifa za nyuma zimetolewa ni kwamba huwezi kutazama mahindi na kusema kwamba yana sumu kuvu lazima uwe na uwezo wa kuchunguza,” amesema Sillo.
Sillo amesema kutokana na athari za sumu kuvu kwa afya ya binadamu, TFDA imechukua hatua mbali mbali ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara na umuhimu wa kutunza mahindi ili kuepukana na maradhi yatokanayo na tatizo hilo.
Mkurugenzi wa usalama wa chakula wa TFDA, Raymond Wigenge ameanisha mambo manne yanayotegenezewa miradi kwa ajili ya utekelezaji.
Mambo hayo ni uelimishaji jamii, teknolojia, tafiti mbalimbali, na sera mahususi zinazolenga kushughulikia tatizo.
Wigenge amesema mazingira yenye unyevunyevu ni rahisi kuzalisha fangasi wanaosababisha t sumu kuvu na amewataka wananchi kuhifadhi nafaka katika mazingira makavu.



Comments